Mama Regina Lowassa afuturisha watoto wanaoishi katika mazingira magumu na wanawake Dar es Salaam

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Katika kuonyesha mshikamano imara na upendo ndani ya jamii ya Kitanzania, mke wa Waziri Mstaafu Edward Lowassa, Mama Regina Lowassa jana Jumanne 05/07/2016 amefuturu na watoto Yatima na Wanawake kutoka maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam na viungwa vyake ambao wamewakilisha Wanawake wenzao wa Dar es salaam na Tanzania kwa ujumla.

Akiongea mama Regina Lowassa baada ya futari amewashukuru Wanawake wote waliojitokeza kushirikiana nae katika futari maalum na watoto Yatima.

"Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa nguvu na kufanikiwa kujumuika pamoja katika hiki kidogo, nikiwa na watoto wangu hawa na wanawake wenzangu wa Dar es salaam, kwani mmeacha shughuli Zenu, pamoja na foleni kali ya Dar es salaam, mkaamua kuja kushiriki futari hii ,nawashukuru sana" Amesema Mama Regina Lowassa.

"Niliona nikiwa na watoto pekee yao bila wale ambao ndio mama zao, Dada zao, shangazi isingekuwa na afya sana, nilitamani niwe na wanawake wake wote wa Dar es salaam na Tanzania lakini isingewezekana ni wengi mno lakini ninyi ni wawakilishi wao, mkawashirikishe yale mazuri tuliyozungumza hapa, hapa tupo Watanzania, dini zote, makabila yote, bila kujali rangi, itikadi sisi wote ni Watanzania" Ameongeza.

Mama Lowassa amesisitiza upendo ndani ya jamii ingawa changamoto hazikosekani ambazo muda mwingine hugawa watu, binadamu hukosea lakini hakuna budi kusameheana inapobidi, wanawake wanachangamoto nyingi lakini wanawake wametakiwa kusimama imara na kuzikabili, na kila wakati amesisitiza mwanamke ndiye nguzo kuu katika ngazi ya familia na jamii nzima hivyo amewataka wanawake kushirikiana katika kila jambo, ikiwemo shida na raha.

Pia ametumia fursa hiyo kuwatakia Eid Mubarak Waislamu wote, amewataka waendeleze mambo mema ambayo ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, kwa kuwapenda wengine.
 

Attachments

  • IMG-20160706-WA0006.jpg
    IMG-20160706-WA0006.jpg
    75.9 KB · Views: 75
  • IMG-20160706-WA0008.jpg
    IMG-20160706-WA0008.jpg
    78.4 KB · Views: 77
  • IMG-20160706-WA0010.jpg
    IMG-20160706-WA0010.jpg
    86.7 KB · Views: 72
  • IMG-20160706-WA0009.jpg
    IMG-20160706-WA0009.jpg
    101.8 KB · Views: 73
  • IMG-20160706-WA0005.jpg
    IMG-20160706-WA0005.jpg
    93.3 KB · Views: 75
  • IMG-20160706-WA0003.jpg
    IMG-20160706-WA0003.jpg
    78.5 KB · Views: 77
Pongezi Mama Yetu Regina Lowassa Mungu atazidi kuwalipa mema Na Mpendwa Kamanda wetu aliyekubali kutukana Na vijana wa Lumumba bila hatia yoyote ila wakumbuke Malipo no hapa hapa Duniani Viva Lowassa viva kamanda
 
Pongezi Mama Yetu Regina Lowassa Mungu atazidi kuwalipa mema Na Mpendwa Kamanda wetu aliyekubali kutukana Na vijana wa Lumumba bila hatia yoyote ila wakumbuke Malipo no hapa hapa Duniani Viva Lowassa viva kamanda
Teuzi zimewafanya wameanza kumbuana buku saba
 
Hawana roho hiyo. Jambo hili ni gumu ni lazima lijengeke kwa n dani ya moyo wa mtu siyo la kuiga
 
HAKIKA anastahili PONGEZI. Nimeona watu wengi maarufu wakialika watu futari akiwepo Mh. Rais Na Mkuu wa Mkoa. Hakuna hata mmoja ambaye aliwafikiria hawa watoto. Unawaalika walionacho huku ukiwasahau waliofunga na bado hawana hakika ya kupata walau futari.

MUNGU AKUBARIKI MAMA LOWASSA
 
safi sana Mama. ccm waige mifano kama hii.

swissme
Mkuu Swissme, kwa dhati kabisa naungana na wewe katika kumpongeza mama Lowassa kwa tendo hilo la ukarimu. Nampenda na kukubaliana sana huyu mama.

Hata hivyo nina tatizo na hapo kwenye "ccm waige mifano kama hii". Kwa kweli kama alivyosema mchangiaji mmoja, jambo hili si la kumuiga fulani bali ni vema sana litoke moyoni kwa mtu mwenyewe. Pia kwa kuwa tendo lenye lilifanywa na mama Lowassa na siyo taasisi au chama, nadhani si sahihi kusema chama fulani kiige.
 
hongera mama lowassa, first lady wa mioyo yetu!! ila pesa mlizotumia kuitafuta ikulu ni nyingi sana, ni bora mngetoa sadaka kwa hao yatima maana ikulu mtaishia kuiona kwenye TV na magazeti!!
 
Back
Top Bottom