MWANZO WA MAHUSIANO
Jamaa mmoja alikuwa anapiga tempo shule fulani mwaka Jana 2016 baada ya kuhitimu kidato cha sita katika mchepuo wa PCB. Wakati akiwa shuleni hapo alikaona matoto kazuri na kukapenda. Watoto hao 20&18 wakaanza mahusiano na mwezi October jamaa akajiunga UDSM. Binti baada ya mtihani wa taifa alifukuzwa kwao na kuelekea Arusha.
Huko A.town alienda kufanya kazi za ndani. Kwakipindi hicho akiwa huko alikuwa akiwaziliana na baba yake tu. Mama na baba yake walitengana na yeye baada ya kuonekana ni team baba mama alimtimua na kubaki na wanaomuunga mkono. Sasa dogo maisha ya ufanyakazi yakamshinda na kuamua kutimkia dar.
BINTI NDANI YA DAR
Binti aliingia dar na kufikia kwa ndugu wa mama aliyempa siku tano tu za kukaa pale. Katika siku hizo alifanikiwa kupata marafiki waliokuwa wanafanya mafunzo ya kuigiza. Baada ya muda kama miez kadhaa mpaka April a
Ndipo akapajua anapokaa mpenzi wake. Kutokana na yeye kuchemka baada ya kufeli aliamua kumganda jamaa kisawasawa. Basi jamaa akakubali kuishi na binti kwenye room alilopanga kitaa(off compus).
Mwezi July walianza safari ya kurudi kijijini baada ya chuo kufunga. Yeye na binti wanatokea kata moja kasoro vijiji tu. Sasa hapa ndio penye mgogoro hasaaa!!
VIJANA WAREJEA NYUMBANI
Walirudi na kufikia kwa wazazi wa jamaa kwasababu hana nyumba pia ni mdogo (21 yrs) na binti (19). Sasa baada ya kufika wazazi wakaelezwa kuwa yule ni mchumba wake na alikuwa akiishi nae Dar. Wazazi wakaona isiwe shida wakamkubali binti na kumpokea kama mkamwana wao.
Tar 2 July, waligafuta washenga na barua ya posa ikapelekwa. Ile barua ilipelekwa kwa baba wa binti na mama aliitwa kuijadiri barua ile.
Kutokana na mgogoro kati yao mama alisema atatoa maoni yake siku inayofuata.
Baada ya kufika nyumbani alikaa na watoto wanaomuunga mkono yeye na wakamwambia asikubari Dada yao aolewe(wao wameoa na kuolewa). Mama pia kaongea na ndugu wakamwambia asikubari binti atapata taabu tu kwasababu kijana ni wa familia ya hari ya chini sana.
Kutokana na maoni hayo alimpigia sim binti na kumtisha kuwa asipobadili msimamo asimtambue kama mama yake. Binti akapuuza vitisho na kumweleza juu ya hisia zake.
HIRA ZA MAMA MKWE
Kutokana na yeye kuwa nesi alichukua kadi ya clinic na kuikopi ile original ila tarehe na mwaka vikabadilishwa. Kadi hiyo ilionesha binti amezariwa 2001 na kwamba anamiaka 16. Pia kutokana na yeye kuwa miongoni mwa watu wanaoshughulikia masuala ya akina mama na haki za mtoto wa kike alipeleka kesi halmashauri ya wilaya na kufungua kesi ya ubakaji na utoroshaji/utekaji kwa kijana, mzazi mwenzie alituhumiwa kuozesha binti chini ya miaka 18, washenga na wazazi wa kijana nao walihusishwa na madai hayo.
Polis walipewa taarifa na kuamriwa kumkamata kijana na wazazi wake. Sasa polis walipofika walimkuta mdogo mtu /wifi mtu na kumshikiria yeye kama mateka. Baada ya wazazi kufika kituoni wakasomewa mashtaka na kuahidi kurudi siku ya pili wakiwa na binti kama shahidi mkuu.
MWISHO WA UBAYA......
Kabla ya siku ya mashauri polis walifika shuleni alikokuwa anasoma binti na muchukua leaving certificate, walifika kituo cha afya na kuchukua baadhi ya data na kuonana na nesi aliyemhudumia mama huyo akijifungua na baadhi ya majirani na ndugu.
Siku ya mashauri binti alieleza mwanzo mwisho na mpaka baadhi ya SMS na sauti zilizorekodiwa zilitolewa. Polis pia wakatoa leaving certificate ikaonesha binti amezaliwa 1998 na sio 2001.
Kesi ikageuka na yeye kuonekana ameghushi nyaraka za serikali, akaomba msamaha mpaka akatia huruma. Akapigwa fain ya laki tano kufuta mashtaka kituo cha polis na sasa anahangaika kufuta mashtaka ngazi ya wilaya.
Sent from my VFD 301 using JamiiForums mobile app