Mama mkwe ananing'angania


Daah ila hapo kwa mdogo wake mm naona hapafai bana kwa sababu huyo mkubwa wake lazima atawaletea zengwe tu iwe isiwe...
 
Nakushauri achana kabisa na hio familia.Mamamkwe anakubebembeleza uchukue mdogo wake kwa kua hua unaprovide vijicent kwenye hio familia, anachosema mamamkwe kua huyo bint anakupenda ni uongo, angekua anakupenda asingekua anakutumia hizo picha alizopiga na wanaume wake huko kenya.
 
Hivi wewe umesoma chuo kipi? Mwanafunzi wa chuo ndio anaandika namna hii?

Hicho ni chuo cha makanjanja na wazee wako walipoteza wakati na fedha zao bure kukupa elimu ambayo huwezi kuitumia hata kwa kuandika sawa.

Kwa hiyo elimu yako inapimwa kwa uwezo wa kuandika?Kipi hakijaeleweka hapo?Au we ni mwalimu wa somo la mwandiko umekuja kunisahihisha upo kwa ajili ya kukagua maandishi na si kutoa ushauri?Nakuomba utoe ushauri wako kwa kile ulichoelewa na si vinginevyo! Au we ni MMBURU mwenye tabia hiyo nloandika. Hapo juu?
 

Yani hata we mwenyewe nahisi kama hujielewi, na usipoangalia utaweza jwrli kuishia kumuoa huyo mdogo wake au worse zaidi kumrudia huyo dada mtu, ndoa si lelema ndugu na ukichemsha sasahv jiandae kuishi kwa majuto for the rest of ur life ushauri kua kwanza kiakili na kata mawasiliano na huo ukoo wa huyo
dada anza upya
 

Ushauri wangu wa kwanza; Andika kama mwanazuoni aandikavyo kama unavyojidai kujisifu humu eti mlikutana chuo. Anzia kwa ku edit maandiko yako yasomeke, kama unajuwa maana ya ku edit.

Maandiko yako na msomi wa chuo ni vitu viwili tofauti. Kama kweli u mwanachuo basi nawahurumia wazee wako waliokugharamia, hukusoma ipasavyo.
 
Mama mkweeee hatareeee, kajitoa kweli fahamu yaani yuko radhi mabinti wake kuvurugwa na mtu mmoja😛hoto:..Na wewe naona ushaingia tamaa kwa mdogo wake lakini ipo pouwaaa kila la kheri kaoe sema pimeni afya kwanza ...!¬
 
hadi maza anakupa bonus uoe mdogo mtu?
kweli mtoto wa kike mtaji....
 
We mwenyewe huna akili ya kufikiria?

Unadhani ni sawa kupewa mdogo mtu?
 
Hata Kama huyo mama alikupenda sana kama mkewe mtarajiwa...napata mashaka anapomkuwadia bintiye mwingine. KUNA OBJECTIVES anataka ku achieve take care Kijana. Nibora angeishia kukuomba urudiane Ma huyo ex wako kuliko anachofanya sasa! Hakuna kupendwa hapo ndugu, wameona huna mkono wa birika sasa inakuwa tabu kupoteza
 
Hata Kama huyo mama alikupenda sana kama mkewe mtarajiwa...napata mashaka anapomkuwadia bintiye mwingine. KUNA OBJECTIVES anataka ku achieve take care Kijana. Nibora angeishia kukuomba urudiane Ma huyo ex wako kuliko anachofanya sasa! Hakuna kupendwa hapo ndugu, wameona huna mkono wa birika sasa inakuwa tabu kupoteza resource Kama wewe. Achana huko Kwa mdogo mtu Kama Utaamua kurudiana na huyo wa awali ni uhuru wako. Kumbuka kuna alarm haPo
 
Hukujua Kama bi Desii wakati mnaanza ku date?
Hata hivyo Kabila lake sioni kama linamaana as mapenzi hayana Kabila, rangi, kimo, uwezo, umri wala saizi ya umbo!
 
Hili litakuwalimesoma boys, achana na hiyo familia kabisa.
 

Nna-uhakika hujawahi kuusikia msemo "Pen is mightier than the sword".

Utafute kwa kutumia google uujuwe maana yake ni nini, itakusaidia.

Faidika na Darsa la FaizaFoxy.
 
Hujitambui kimapenzi,hujui hisia zako zikoje,

Fanya maamuzi uachane na hiyo familia,Ka ukijua huruma huzaa dhambi sasa kazi kwako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…