Wacha utani bana, wewe kwa akili zako unategemea huyo JPM angekubali kupokeza madaraka kwa Lissu hivi hivi tu, hilo hata Lissu alilifahamu, nafikiri Lissu nia yake kuu ilikua kumtikisa JPM na kumuonyesha yuko uchi na kwamba nchi ina matatizo na uongozi wake hivyo akubali kuchutama na kurekebisha.
Na wandani na wapambe wa JPM walifahamu nia ya Lissu, hivyo ikawa mwendo wa kusindika ili kuufuta upinzani kabisa. Unajua ukiwa kiongozi kisha uambiwe waliopiga kura idadi yao ni milioni ishirini, ila wewe umeshinda kwa kura milioni kumi na moja na kwamba milioni tisa hawakukupigia, hawakutaki, unakaa mkao wa kujua kuna watu milioni tisa wapo ndani ya nchi hawakutaki kabisa, kwa hivyo utarekebisha, ila pale unaambiwa asilimia 98% walikupigia, aisei utatembea kifua mbele.