Mama huyu kipofu kanishangaza

Mama huyu kipofu kanishangaza

Last week nilienda kuwatembelea wazee home. Nikakuta jirani kuna mama mmoja kipofu, ni mwalimu wa primary kahamia pale. Ana watoto watatu wa kike ila wawili hawapo na siwajui pale anakaa na binti yake mmoja. Sasa hiyo siku yule binti nadhani alikua ametoka, ghafla luku iliisha. So mama baada ya kujua ni luku akanunua pale kwa wakala, then akaniomba mie nikamuwekee.

Nikiwa niko sebuleni naingiza ile Luku, mama yeye alikua amekaa jikoni anakata mboga. Kwa dirishani nikamuona binti mmoja (simjui) anaingia getin kwa kunyata. Akaja kwa kunyata mpaka kwenye huu mlango wa sebuleni. Akanikuta mie namshangaa akanifanyia shiiii na kidole mdomoni, ishara nisiseme kitu niendelee na shughuli zangu.

Akapita sebule akawa anafata ile korido ili afike jikoni kwa mwendo wa kunyata. Akawa katikati hajafika hata mlango wa jiko mama kule jikoni akasema kwa nguvu, NANI ANANYATA? Nkashangaa sana. Binti yule akasogea had mlango wa jikoni. Akawa anamuona mama yake, na mama anaangalia huu upande wa mlangoni, lakini ndo haoni. Mama akaita jina langu, nikaitaka nikiwa sebulen, akauliza nani huyu kaja kwa kunyata jikoni? Nikiwa nmeduwaa sijui nmjibuje mama akataja jina la yule binti, Mwanangu Vero (sio jina halisi), yaani umekuja bila taarifa na umefika kwa kunyata au ndio sapraizi?

Binti alivosikia mamake kamtaja jina, kamjua bila hata kumgusa akaenda kumkubatia mama yake akaanza kulia. Nikaja kujua ni mtoto wa kwanza wa huyu mama aliondoka since 2019 feb. Karudi ghafla bila taarifa. Lakini mama yake kipofu kamjua bila hata kumgusa.

Walipokumbatiana mama akamwambia binti yake umenenepa, baada ya kumpapasa usoni,

Masikini....damu nzito♥️
 
Vipofu wana Uwezo Mkubwa sana wa Kutambua bila Kuona
Kabisa. Kuna wengine huwa wanatembea huku wanatoa sauti fulani, kama wana-click clich ulimi wao. Kutokana na hiyo sauti inavyosafiri na kurudisha mwangwi wanajua sehemu zenye vikwazo na sehemu sahihi za kupita. Unakuta mtu anajua mbele kuna ukuta au mtu nk.
 
Duh...Mungu kweli hawezi kukuacha ukataabika moja kwa moja
 
kuna mzee wa kimasai kule longido ni kipofu na ana ngombe km elfu hivi.ajabu ngombe 1 tuu au ht akizaa asione ndama anaulizia kwamba ngombe flan alizaa mbona mtoto hajaingia zizini
 
Last week nilienda kuwatembelea wazee home. Nikakuta jirani kuna mama mmoja kipofu, ni mwalimu wa primary kahamia pale. Ana watoto watatu wa kike ila wawili hawapo na siwajui pale anakaa na binti yake mmoja. Sasa hiyo siku yule binti nadhani alikua ametoka, ghafla luku iliisha. So mama baada ya kujua ni luku akanunua pale kwa wakala, then akaniomba mie nikamuwekee.

Nikiwa niko sebuleni naingiza ile Luku, mama yeye alikua amekaa jikoni anakata mboga. Kwa dirishani nikamuona binti mmoja (simjui) anaingia getin kwa kunyata. Akaja kwa kunyata mpaka kwenye huu mlango wa sebuleni. Akanikuta mie namshangaa akanifanyia shiiii na kidole mdomoni, ishara nisiseme kitu niendelee na shughuli zangu.

Akapita sebule akawa anafata ile korido ili afike jikoni kwa mwendo wa kunyata. Akawa katikati hajafika hata mlango wa jiko mama kule jikoni akasema kwa nguvu, NANI ANANYATA? Nkashangaa sana. Binti yule akasogea had mlango wa jikoni. Akawa anamuona mama yake, na mama anaangalia huu upande wa mlangoni, lakini ndo haoni. Mama akaita jina langu, nikaitaka nikiwa sebulen, akauliza nani huyu kaja kwa kunyata jikoni? Nikiwa nmeduwaa sijui nmjibuje mama akataja jina la yule binti, Mwanangu Vero (sio jina halisi), yaani umekuja bila taarifa na umefika kwa kunyata au ndio sapraizi?

Binti alivosikia mamake kamtaja jina, kamjua bila hata kumgusa akaenda kumkubatia mama yake akaanza kulia. Nikaja kujua ni mtoto wa kwanza wa huyu mama aliondoka since 2019 feb. Karudi ghafla bila taarifa. Lakini mama yake kipofu kamjua bila hata kumgusa.

Walipokumbatiana mama akamwambia binti yake umenenepa, baada ya kumpapasa usoni,
Huwa kuna jicho la tatu, kitaalamu linaitwa hypothalamus!
 
Daah hii imenikumbusha kuna siku nilimuona kwa mbali mzee mmoja alikuwa pekeake na zile fimbo nyeupe zinazotumiwa na vipofu alikuwa anatembea anaomba pesa kwa watu anaopishana nao.

Sa bwana mm kumuona anakuja upande wangu nikaamua kutembea polepole kwa kunyata nikijua hatajua..ebwanaee nilivyomkaribia nikampita shaah daah sikuamiini yule babu aligeukia ule upande wangu akaniongelesha " wew kijana .....". Daah hadi leo sijaelewa yule dingi alikuwa msanii wa mjini au ni kipofu OG.
 
Mkuu wapo vipofu hadi gari wanaendesha. Mungu ni wa ajabu
 
Kabisa. Kuna wengine huwa wanatembea huku wanatoa sauti fulani, kama wana-click clich ulimi wao. Kutokana na hiyo sauti inavyosafiri na kurudisha mwangwi wanajua sehemu zenye vikwazo na sehemu sahihi za kupita. Unakuta mtu anajua mbele kuna ukuta au mtu nk.
Sikuwahi kujua kazi ya zile sauti nina baba mdogo wangu haone since azaliwe hua anatoa hyo sauti na anatufaham vizuri kweli akiwa pia na ile fimbo yake nyeupe bas anaenda popote bila msaada

Kuna siku kitunguu kilianguka kutoka kwenye ungo alienda kukiokote kama mtu mwenye macho mazima kabisa.
 
Kuna mama kipofu anajua hadi rangi ya mtu kama n mweupe au mweusi kwa kumgusa tu
 
Sikuwahi kujua kazi ya zile sauti nina baba mdogo wangu haone since azaliwe hua anatoa hyo sauti na anatufaham vizuri kweli akiwa pia na ile fimbo yake nyeupe bas anaenda popote bila msaada

Kuna siku kitunguu kilianguka kutoka kwenye ungo alienda kukiokote kama mtu mwenye macho mazima kabisa.
Ndugu yangu binadamu tuna uwezo mkubwa sana kwenye milango ya fahamu ila sehemu kubwa ya uwezo imefifia au kufa kabisa kutokana na kutoitumia.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom