Mama huyu kipofu kanishangaza

Mama huyu kipofu kanishangaza

DAVID PALMER

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2020
Posts
323
Reaction score
1,625
Last week nilienda kuwatembelea wazee home. Nikakuta jirani kuna mama mmoja kipofu, ni mwalimu wa primary kahamia pale. Ana watoto watatu wa kike ila wawili hawapo na siwajui pale anakaa na binti yake mmoja. Sasa hiyo siku yule binti nadhani alikua ametoka, ghafla luku iliisha. So mama baada ya kujua ni luku akanunua pale kwa wakala, then akaniomba mie nikamuwekee.

Nikiwa niko sebuleni naingiza ile Luku, mama yeye alikua amekaa jikoni anakata mboga. Kwa dirishani nikamuona binti mmoja (simjui) anaingia getin kwa kunyata. Akaja kwa kunyata mpaka kwenye huu mlango wa sebuleni. Akanikuta mie namshangaa akanifanyia shiiii na kidole mdomoni, ishara nisiseme kitu niendelee na shughuli zangu.

Akapita sebule akawa anafata ile korido ili afike jikoni kwa mwendo wa kunyata. Akawa katikati hajafika hata mlango wa jiko mama kule jikoni akasema kwa nguvu, NANI ANANYATA? Nkashangaa sana. Binti yule akasogea had mlango wa jikoni. Akawa anamuona mama yake, na mama anaangalia huu upande wa mlangoni, lakini ndo haoni. Mama akaita jina langu, nikaitaka nikiwa sebulen, akauliza nani huyu kaja kwa kunyata jikoni? Nikiwa nmeduwaa sijui nmjibuje mama akataja jina la yule binti, Mwanangu Vero (sio jina halisi), yaani umekuja bila taarifa na umefika kwa kunyata au ndio sapraizi?

Binti alivosikia mamake kamtaja jina, kamjua bila hata kumgusa akaenda kumkubatia mama yake akaanza kulia. Nikaja kujua ni mtoto wa kwanza wa huyu mama aliondoka since 2019 feb. Karudi ghafla bila taarifa. Lakini mama yake kipofu kamjua bila hata kumgusa.

Walipokumbatiana mama akamwambia binti yake umenenepa, baada ya kumpapasa usoni,
 
Kiungo kimoja kiki cease kufanya kazi hupelekea vingine kuwa active zaidi kuliko mwanzo ili kufidia mapungufu,,huyo mama macho yamekufa ila masikio,pua,ngozi etc,vinafanya kazi ove rtime ku offset mapungufu ya macho
 
Asee Acha tuu
Kipofu Mungu huumpa njia mbadalaa


Ila huwa nakuwa na Shaka na wale wanaomba omba bara barani
 
Mwanangu Vero (sio jina halisi), yaani umekuja bila taarifa na umefika kwa kunyata au ndio sapraizi?

Binti alivosikia mamake kamtaja jina, kamjua bila hata kumgusa akaenda kumkubatia mama yake akaanza kulia
Huyo mama made my eyes wet
 
Si ajabu anawajua wanawe kwa harufu fulani. Ila kwa kujua mtu ananyata, inaelekea ana uwezo mkubwa sana wa kusikia.
 
Si ajabu anawajua wanawe kwa harufu fulani. Ila kwa kujua mtu ananyata, inaelekea ana uwezo mkubwa sana wa kusikia.
Kusikia na harufu. Sababu alisikia tuu harufu ya mwanae.. akamtambua
 
Binadamu yoyote ana harufu yake mwenyewe yaani ya kipekee haiingiliani na ya mwingine ndiyo maana mbwa anamtambua binadamu kwa harufu.

Na huyo mama kapewa uwezo wa kipekee kutambua mtoto wake au mtu wa karibu yake kwa harufu.
 
Uzi umenikumbusha rafiki yangu mmoja mwanasheria kipofu genius...
 
ndio kuna manyuzi huko jamii inteligent.

namna ya kuamsha mlango wa sita wa fahamu,ni kama unaa act huna hii mitano,unaamsha huo wa 6.ukiamka unakuwa na machale mbaya mbovu.

hao vipofu,na wasiosikia,huwa mlango wa 6 unaamka automatic kureplace huo mmoja.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom