Kwanza pole kwa majereha uliyoyapata kwa jamaa zako, hadi ukafikia kutomwamini mtu unayelala naye kitanda kimoja. Naomba kuuliza tena. Wewe unamwamini mama yako kuliko unavyomwamini mkeo?? Yani moyo wako unafunguka kwa mama yako kuliko kwa mkeo?? Sio lazima ujibu hapa jijibu hata moyoni. Halafu fikiria maisha ya mkeo wakati ambapo labda Mungu ameamua kukuita kabla yake.