Mama Adai Shetani Lilimtuma Amchinje Mwanae | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mama Adai Shetani Lilimtuma Amchinje Mwanae

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Jul 28, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jul 28, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Polisi wakifanya uchunguzi kwenye nyumba ya Otty Sanchez ambaye alimuua mwanae akisema kuwa aliambiwa afanye hivyo na shetani Tuesday, July 28, 2009 4:58 AM
  Mama mmoja wa nchini Marekani amemuua mtoto wake mchanga wa wiki tatu na nusu akidai kuwa shetani alimtuma afanye hivyo. Polisi wa Texas nchini Marekani walisema kuwa walimkuta mtoto mchanga mwenye umri wa wiki tatu na nusu akiwa amechinjwa na mwili wake kukatwakatwa kwa kisu na mama yake ambaye alikuwa akipiga kelele kuwa amemuua mtoto wake baada ya Shetani kumwambia afanye hivyo.

  Mama huyo , Otty Sanchez, 33, wa San Antonio, alichukuliwa na kuwahishwa hospitali hali yake ikiwa mbaya kutokana na majeraha aliyopata kwa kujichoma na kisu kifuani na tumboni, alisema msemaji wa polisi wa San Antonio, Joe Rios.

  Polisi walikuta jambia, kisu kidogo cha jikoni na kisu kinachotumika kukatia miwa ambavyo vyote mama huyo alivitumia katika mauaji yake hayo.

  Polisi waliwakuta pia watoto wawili kwenye nyumba hiyo ambao walikuwa salama hawajadhuriwa na mama huyo.

  "Polisi walipofika nyumbani kwake, alikuwa amekaa kwenye sofa huku akipiga kelele ' Nimemuua mtoto wangu'" alisema msemaji huyo wa polisi.

  "Alisema kuna mtu au kitu kilimwambia afanye hivyo, alidai kusikia sauti zikimwambia afanye hivyo na kutufanya tuamini kuwa atakuwa na matatizo ya akili".

  "Kichwa cha mtoto wake kilionekana wazi kikiwa kimetenganishwa na kiwiliwili".

  Polisi walisema kuwa mama huyo baadae aliwaambia polisi kuwa shetani alimwambia amchinje mtoto wake.

  Mama huyo atafunguliwa mashtaka ya mauaji.

  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsId=2649074&&Cat=2
   
Loading...