Malumbano ya Hoja: Agizo la Rais vijana kuacha uzurulaji na kufanya kazi, je limewekewa mikakati?

Jumaaly

Member
Sep 5, 2015
74
21
TAARIFA
Leo usiku katika kipindi cha Malumbano ya Hoja kupitia kituo cha ITV, kijana mwenzetu Mwenyekiti wa Jukwaa Huru la Wazalendo comrade Ally Salum Hapi amealikwa miongoni mwa wageni wa meza kuu katika kujadili mada isemayo

"AGIZO LA RAIS VIJANA KUACHA UZURULAJI NA KUFANYA KAZI, JE LIMEWEKEWA MIKAKATI ENDELEVU?

Shime vijana wote Wazalendo tutazame mjadala huo muhimu kwa mustakabali wa maisha yetu kama vijana nchini.
 
hivi unakwenda kulima wapi, kwa gharama zipi, kulala wapi, kutibiwa wapi, na unalima nini, huko wanakotaka kutupeleka hakuna watu ni mbugani au watajenga kambi mpya za wazururaji?
mjini ndio kila kitu leo hela huna kesho oya oya.... kama wameshindwa kuziondoa boda boda mjini kwa 100% wataweza wazururaji mambo mengine wanazingua...
mfano serikali ikasema atakaekwenda kulima atapewa posho ya laki 5 nawaambia watajazana ndugu na jamaa huko maporini na wababaishaji wakabaki mjini si tupo
 
Kwa sasa sio rahisi kutekeleza agizo hilo na hasa ukizingatia kuwa wafadhili wamekata misaada kwa nchi yetu, tutegemee ugumu wa maisha
 
Back
Top Bottom