Malipo manono tume ya katiba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Malipo manono tume ya katiba

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kakulwa P, Jul 2, 2012.

 1. Kakulwa P

  Kakulwa P JF-Expert Member

  #1
  Jul 2, 2012
  Joined: Feb 8, 2012
  Messages: 200
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu wanaJF Salam,
  Nimesikia mwenyewe kauli ya Balozi Sefue akitaja wajumbe wa Tume ya Kuratibu maoni ya Katiba watavyonufaika wakati wa utekelezaji wa kazi zao, alitaja yafuatayo kwa kila mjumbe.

  1. Kupewa Gari Jipya
  2. Kupewa Nyumba

  Lingine nimesikia kuwa wanalipwa posho ya shilingi 450,000/- kila siku.
  Ndugu zangu kamati hii ina wajumbe 30 toka maeneo ya Jamhuri yetu ya Muungano, lakini pia hawa wajumbe wametoka kwenye taasisi mbalimbali kunazia bungeni, vyuoni, vyama vya siasa na maeneo mengine ili mradi wamekidhi sifa ambazo Marais wetu aliona zinafaa.

  1. Naanza kuhoji juu ya kupewa magari ya tume, mimi ninavyowajua wajumbe wote wa Tanzania bara wanayo magari yao wanayoyatumia kila siku, kwa nini serikali haikupenda kuwawekea mafuta tu ili waweze kwenda kazini kila siku badala ya kuingia gharama kubwa za kununua magari mapya. Hapo tungepunguza fadha nyingi na kuzifanyia shughuli nyingine ya maendeleo ya wananchi wetu.

  2. Wajumbe wote waliopo Tanzania bara wanazo nyumba zao wanapoishi, sasa hizi nyumba wanazopewa na serikali hazina ulazima labda kwa wale wajumbe wa Tanzania visiwani ambao watakuja kwa kazi hizi maalum.

  3. Posho 450,000/-wa siku ni kiasi kikubwa mno kulingana na maisha duni ya wananchi kwenye nchi hii, nilikuwa na matarajio makubwa kuwa wajumbe hawa wangekataa kiasi hicho kikubwa lakini wamekaa kimya tangu walipotangaziwa wanachokiita NEEMA KWAO.

  WanaJF wenzangu kwa mfumo huu wa kutanguliza maslahi manono kwa wajumbe wa Kamati ya Katiba, na mkiangalia muda ambao wameupanga, masaa matatu kila Tarafa kwenye kutoa maoni kutoka kwa wananchi tunatarajia KATIBA YA WATANZANIA? Nalileta hili ambalo mimi nimeona kama kikwazo ili tusaidiane kulisema.
   
 2. b

  bgmy Member

  #2
  Jul 2, 2012
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hakuna kikwazo chochote...waacheni wafanye kazi yao ngumu ktk mazingira mazuri ili waweze kutuletea kinachosubiriwa na wengi...usiangalie kiwango angalia kazi waliyopewa au majukumu waliyopewa....mboni weatanzania mnashangaza sana...sasa mlitaka walipwe kiwango gani?? halafu mje kuzungumza mnalolitaka??? watanzania acheni majungu
   
 3. Tetty

  Tetty JF-Expert Member

  #3
  Jul 2, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 25,559
  Likes Received: 16,530
  Trophy Points: 280
  Serikali yetu imeshindwa kuboresha mazingira ya hospitali zetu.Tuangalie kwa mwezi Mjumbe mmoja anapewa hivi:
  Mjumbe mmoja kwa mwezi 450,000x30=13,500,00
  Wajumbe 30 kwa mwezi 13,500,000x30=405,000,000
  Posho kwa mwezi na sijui hawa watu watatumia muda gani.
  Tumekwisha.....................Ni bora mwanasiasa kuliko mtanzania aliyewapa kura zetu,Inaumiza sana!
   
 4. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #4
  Jul 2, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,896
  Likes Received: 5,358
  Trophy Points: 280
  jk kafanya makusudi kuwajaza hayo maposho ili watu wasilalamikie mabilioni anayotumia na misafari yake useless..
   
Loading...