Malipo Internship ya Udaktari

Malipo Internship ya Udaktari

emmadeclassic

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2015
Posts
304
Reaction score
133
Najiuliza tu hivi serikali inakuaga na bajeti ya intern Doctors au hua ni mpaka wazitafute, kama zipo kwenye bajeti kwanini zisitolewe on time? Imagine tupo hospitalini toka 10 november hapo tulitumia zaidi ya malaki kufata provisional registration MCT dodoma (mzigo kwa wazazi).

AUkizingatia mazingira kwa wengi wetu ni mapya tulipanga kujiegesha kwa kulipa mwezi mmoja sasa umeisha na hakuna dalili yoyote ya kupata, serikali kwanini msitoe hela mapema tujikimu..chakusikitisha zaidi ni mwezi sasa hatujapewa logbook ambazo tulizilipia 10k, huo usajili tu 40k ,nauli kama upo rukwa ni zaidi ya 100k.
 
Intern sio mwanafunzi
Ndio maana nilisema turudi nyuma kidogo, Intern si alikuwa mwanafunzi ?

Kulitakiwa kuwe kuna "smooth transition" kutoka hatua ya uanafunzi mpaka kuwa intern na kupata kibali cha kudumu cha kutibu, ni rahisi kupigia kelele mkiwa chini ya mwavuli wa uanafunzi kabla ya kutawanywa huko kwenye vituo mbali mbali na majukumu mbali mbali sauti inaweza isiwe na nguvu ya kutosha. Ni maoni yangu tu mlioko kwenye fani mnaelewa zaidi !
 
Pole sana mkuu, huwa inachukua zaidi ya miezi miwili na huwa haitolewi sababu ya msingi. Mwaka wetu ilitoka tarehe 22 Dec kwa hiyo tulikaa mda mrefu kuanzia tarehe za mwanzo za mwezi october. Kuwa mvumilivu tu pesa itakuja.
 
Back
Top Bottom