Mommadou Keita
JF-Expert Member
- Oct 8, 2013
- 230
- 238
TUMEWAONA na kuwasikia wanasiasa wengi wakishangiliwa kwa nguvu huku wakibebwa mabegani na wananchi wenye matarajio makubwa ya kukombolewa na wanasiasa hao mara baada ya kushinda uchaguzi.
Aidha tumewasikia wanasiasa hao wakitoa ahadi zisizotekelezeka kwa wananchi kwa kuwaambia kwamba watayamaliza matatizo yao ndani ya siku 100 mara baada ya kuchaguliwa kwao.
Kama vile haitoshi, tumewasikia na kuwaona wanasiasa hao wakiingia madarakani na kauli za kutoa misamaha kwa wafungwa mbalimbali wa kisiasa na makosa madogomadogo ya kijamii huku wakitaa kujihusisha na wale waliofungwa kwa rushwa.
Ushawishi wa kauli na matendo hayo ya kisiasa huwa ni kuwafanya wananchi wawaamini kwamba wao ni watekelezaji wazuri wanaoweza kuwapa kile wanachokitaka bila ya kuwadhurumu.
Lakini baada ya siku 100, wananchi wanakuwa wameshajua ni aina gani ya viongozi walionao, hata jitihada na ghiriba walizozitumia kuwadanganya huwa hazina nguvu tena.
Hiyo ni mifano ya wanasiasa ambao kati yao huamini kuwa siasa ni mchezo mchafu, siasa hiyohiyo iliyotapakaa na kuingia katika Nyanja nyingi, hata katika mpira wa miguu maarufu kama soka.
Jumapili iliyopita wadau wa mchezo wa soka waliingiwa na matarajio mapya baada ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF) kumchagua Jamal Malinzi kuwa rais mpya wa shirikisho hilo.
Kila mmoja anaamini kuwa, Malinzi ni mtu sahihi kushika wadhifa huo ulioachwa, Leodger Chilla Tenga na wanaamini kuwa ataweza kulitengeneza soka la Tanzania kwa mafanikio kutokea pale alipoachiwa na mtangulizi wake.
Matarajio ya Malinzi kwa wapenzi wa soka hayatokani na kitu kingine zaidi ya kuamini kwamba kiongozi huyo ni mtu mpya aliyetoka katika kambi tofauti na ile ya Tenga.
Pia, anaaminiwa kwa kuwa ni mtu mwenye msimamo wa kuweza kufanya kile ambacho wengi wanakitarajia kwa kufuata katiba ya shirikisho hilo.
Wengi wanatazamia kwamba ubabaishaji ndani ya TFF utakoma na utendaji utaongezeka katika kulitengeneza soka letu kiasi cha kutufanya tuwe tishio Afrika Mashariki na duniani kwa ujumla.
Kama tulivyozoea kuwasikia wanasiasa wakipewa sifa nyingi, Malinzi naye amesifiwa na kupewa sifa kedekede katika uongozi wake.
Kama wanasiasa wanavyotangaza kutoa siku 100 za neema kwa uongozi wao, Malinzi naye ameshawatangazia wajumbe wa mkutano mkuu na wadau wa soka kwamba ndani ya siku hizo wataanza kuonja mafanikio yake.
Binafsi naamini kwamba wadau watamtathimini kiongozi huyo ndani ya siku hizo, kama atavurunda hawatasita kumwambia ukweli kwa kuwa watajua ni yaleyale ya wanasiasa.
Hali kadhalika, Malinzi amewatoa katika kifungo cha michezo watu waliokuwa hawatakiwi katika soka la Tanzania kama vile Othuman Kazi na Michael Wambura na kumfungulia mwamuzi Martin Saanya na kusisitiza kwamba tusameheane ili tutengeneza upya maendeleo ya mpira wetu wa Tanzania.
Sitaki kuamini na wala sitarajii kumuona Malinzi akifanya kazi ya siasa ndani ya soka, najua anajua anachokifanya na atasimamia haki na usawa kwa maendeleo ya soka letu na kazi yake haitakuwa nguvu ya soda.
Kwani pamoja ule mwonekano wake kwamba ni mwenzetu kwa wale wanaoamini kwamba ni wahanga wa soka la Kitanzania, Malinzi anatakiwa kutambua kwamba akivurunda wadau watambadilikia na kumpa ukweli wa madudu yake.