Ni Bahati Mbaya sana Watanzania wenzangu wengi mlizidiwa na upepo wa Lembeli ambaye sasa kidogo mmeanza kumjua. Wakati ule hamkunipa nafasi ya kunisikiliza. Mungefanya hivyo (kufanya utundu wa kutaka kujua "huyu bwana analalamika hajapata nafasi ya kusema, angepewa nafasi angesemaje?". Kwa kifupi sana, kwenye suala langu, RUSHWA SI KWAMBA MIMI NDIYE NILIPOKEA BALI WALIOKUWA WAKINISAKAMA NDIO WALIOPOKEA WAFANYE WALICHOKIFANYA. Nilisema kuna Mfanyabiashara mmoja aliwafanyia semina na kuwapa posho nono St Gasper Dodoma tar 16/4/2012. Mungejitahidi kufuatilia hiyo tip ingewasaidia sana kutenda haki.
Kwa kuwa na mhimuko na ushabiki, mnajinyima nafasi ya kujua ukweli na hivyo kuishia usemi "UMDANIAYE NDIYE KUMBE SIYE".
Naweza kuthibitisha hivi sasa lobying zinazofanywa (kwa wabunge) na wafanyabiadhara wanaoathirika na maamuzi ya watendaji serikalini ndiyo zinayumbisha na kuchafua Bunge. Anayejidanganya wabunge ni Mashekhe au Maaskofu (kwamba ni wasafi kihivyo) na hivyo kuamini kila wanachokisema basi pole zake.
Rushwa WORKED AGAINST ME. Ningekuwa nimepokea rushwa na kufanya maamuzi yasiyo sahihi yangetokea yafuatayo:-
1. Leo ningekuwa Mahakamani kama Idd Simba au Ekerege, na
2. Maamuzi jiliyofanya yangekuwa yameshabatilishwa.
Chunguzeni kwa nini hayo mawili hayajatokea.
wanaJF hebu mnijuze, pale wizara ya maliasili na utalii kuna nini? Maana kila kiongozi anaeteuliwa huwa hafai na mwishowe huondoka kwa kashfa; kwa kuthibitisha hili hebu tujikimbushe hawa wafuatao:[/COLOR][/FONT][/SIZE]
1. Zhakia Megji – Huyu alituhumiwa kwa kjimilikisha vitalu vya uwindaji isivyo halali
2. Prof. Jumanne Maghembe – Yeye alituhumiwa kufanya mabadiliko makubwa ya wakurugenzi na makamishna pale wizarani kwa utashi wake pia alipandisha bei ya vitalu na wanyama isivyo kawaida.
3. Antony Dialo na Saleh Pamba- Hawa walituhumiwa kwa kufanya biashara ya magogo nje ya nchi ilihali ikiwa imepigwa marufuku na serikali.
4. Shamsa Mwangunga - Yeye na katibu wake Blandina Nyoni walikuwa hawaelewani kabisa kiasi cha kila mmoja kufanyia kazi za serikali nyumbani kisa ni Mwangunga kutuhumiwa kutorosha magogo nje ya nchi bila vibali.
5. Ezekiel Maige- Huyu ndio balaa, licha ya kutuhumiwa kugawa vitalu kwa rushwa na kuwa na ukwasi wa kutisha bado katika kipindi chake wanyama wametoroshwa nje ya nchi huku yeye akijifanya hajui kinachoendelea.
Hapa ndo najiuliza hapa maliasili na utalii kuna nini? Mbona kila anayepelekwa mambo huaribika?