Malezi ya Watoto.

Museven

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2011
Posts
629
Reaction score
452
Heshima kwenu wanajamvi wote.
Naomba maoni yenu kuhusu malezi ya aina hii. Mke wangu ananitia mashaka kwa jinsi anavyowatreat wanangu wawili ambao ni wake pia, matunda ya ndoa yetu. Hana simile, hana upole. Mtoto akikosea yeye ni kufoka, kutukana na kupiga tu. Hana muda wa kuongea na watoto kwa upole na subira wanapokosea. Nikijaribu kumshauri awe na subira, si kufoka na kupiga tu, kukaa nao na kuwaelewesha kwa upole mambo ya nidhamu itasaidia, hunipinga na kusema mimi sijui kulea. (Yeye ana watoto wawili aliozaa na baba mwingine kabla sijamuoa). Nimekuwa nikiwakaripia watoto na kuwachapa kutegemea na ukubwa wa kosa lakini pia huwa naongea na watoto mbele yake kumpa mfano lakini wala hafati. Kwa malezi haya ya mke wangu ya namna hii naweza kupata watoto wenye balanced behaviour kweli? Au ni mimi nakosea? Nini faida au hasara za malezi ya aina hii?
NAWASILISHA!
 
Inasikitisha sana kama mkeo hakuelewi! Kufokea watoto na kuwatolea maneno makali huwafanya wawe waoga na kutojiamini. Njia unayotaka itumike kulea ndiyo sahihi. Je, hao watoto aliowalea ukiwa haupo (kabla ya kuoana) unaridhika na tabia yao? Kama kuna kasoro unazoziona kwenye tabia zao, mwambie hutaki kuona hao uliozaa naye kuwa na tabia kama hizo.

Pole sana ndugu. Baadhi ya wanawake wetu wanajiona wao ndio kila kitu kwenye malezi.
 
Huyo mwanamke ataharibu watoto wenu iyo njia yake siyo sahihi kabisa Nadhani mkeo anahitaji counseling nahisi yeye kwanza asaidiwe haiwezekani kila kitu ni kufoka na makofi jamani.....Kama hakuelewi wewe tafuta mtu ambaye yeye mke Wako anamheshimu umuite amsaidie
 
Hiyo njia anayotumia mkeo sio sahihi, hao watoto watazoea kufokewa na kipigo, baada ya hapo watakuwa masugu hawatasikia lolote. Na watakapo kuja kuwa wazazi nao watakuwa na tabia hiyohiyo ambayo sio nzuri hata kidogo.
 

Asante ndugu kwa maoni yako. Watoto wake wana tabia nisizopenda wawe nazo wanangu. Mkubwa ni mvulana, ni mwoga na hajiamini. Mdogo ni binti, ni mkaidi na mwenye majibu japo mdogo bado.
 

Asante sana ndugu yangu.
 
Imasikitisha kwa kweli, mimi ni muathirika wa malezi ya kufokewa na nimekua mtu mzima sasa nikipambana na kile kilichopandwa kichwani kwangu, nimepoteza kujiamini, kuliko maelezo na hii nimeapa kua haitawafikia wanangu hapo baadae. Ni kitu cha hatari sana katika malezi mkuu pambana uwaokoe wanao maana hao ndio nguzo ya hiyo ndoa yako. Machozi yananilenga kwanini wazazi msijifunze kuwalea watoto kwa njia iwapasayo??????? Whyyyyyy?
 
mm nilikuwa mwalim chin yajwtz 23kj bimlo kama mtoto atalelewa hivyo hataweza kujiamin, kwenye mitihami,maisha,kaz,na kwingineko pole mzee
 
Asante ndugu kwa maoni yako. Watoto wake wana tabia nisizopenda wawe nazo wanangu. Mkubwa ni mvulana, ni mwoga na hajiamini. Mdogo ni binti, ni mkaidi na mwenye majibu japo mdogo bado.
Unaona sasa! Tabia ya huyo binti ya ukaidi na majibu yasiyoridhisha katika saikolojia inaitwa 'defensive attitude'. Kila mara anaona anagombezwa kwa hiyo anatafutab njia za kujihami. Tafuta namna ya kumshauri mkeo asije akaharibu watoto bila yeye kujua.
 
Kwanza huyo mwanamke hajalelewa vizuri. Aitha alilelewa ktkt njia hiyo au mlezi wake hakuwa makini.
Hivi kama mwanamke anamtukana mtoto aliyemzaa mwenyewe anaonesha ishsra gani?
Ndugu yangu, huo ni mzigo na kama hamheshimu mumewe cjui atamheshimu nani!
Cha mcngi ongeza bidii kumpa darasa kwa njia yoyote ile.
 
Oh no. Maybe she is stressed and is taking it out on the kids.
 

pole sana mwanahisa kwa matatizo uliyopitia. Mungu atakusaidia katika mapambano yako, atakushindia. Asante kwa ushauri na ushuhuda wako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…