Huyo mama yeye anaweupe wa asili au wa kununua? baba je yeye ni mweupe? huyo mwanamke atakuwa hana akili huwezi kumbagua mtoto eti kisa rangi na hapo anajitengenezea mipaka kati yake na mtoto isije ikafika ukubwani mtoto anamsaidia sana baba yake mama akaanza kulalamikwa kwa kutengwa au karogwa huyo mama yaani pamoja shida zote analeta ujinga? je mtoto angezaliwa amepungukiwa baadhi ya viungo ingekuwaje sasa!
Wapo watu wa aina hiyo. Niliwahi kuangalia episode fulani hivi ya Tyra Banks kuhusiana na wamama wanaochubua (wanawapaka mkorogo) watoto wao wadogo ili wawe weupe.
Inasikitisha kwamba mwanamke anaweza kufikia hatua ya kumchukia mwanae kwasababu tu ni mweusi lakini jamii inayowazunguka inaweza kuwa imechangia kwa kiasi kikubwa.Malezi tunayowapa watoto wetu, influence tuliyonayo kwa wale wanaotutizama na kutusikiliza ndiyo inayowatengeneza watu either kwa ubaya au kwa uzuri. Huyo anahitaji somo tu, mtu wa kurekebisha na kumbadili mentally.
Wote ni weupe ila hata mtoto ukimtizama sio mweusi vile ni maji ya kunde huo ndio wasiwasi itafika wakati kibao kitageuzwa kwa baba na mtoto wakati mama ndio alitengeneza mwenyewe.