Habar wana JF
Nikiwa kama kijana ambae natafuta mafanikio kwa njia ya halali navuja jasho hasubuhi machana kutwa nikitafuta mafanikio nakujenga msingi wa familia yangu waweze kuishi maisha mazuri yenye furaha ""Pesa ndio sabuni ya Roho""
Hapo hapo naendelea kufanya ibada ili nipate baraka na Neema kutoka kwa mola wangu muumba wa mbingu na ardhi ukiwa mwezi mtukufu wa Ramadhani naomba kuwatakia mfungo mwema waislam wenzangu
Tuendelee kuupa eshima mwezi mtukufu kwani ni mwezi ambao umeshushwa Qruan ndani yake
nisiwachoshe sana naomba niingie kwenye mada husika
Kwasasa nafanya biashara ya Duka la Jumla bidhaa kama Tambi mafuta ya kura sababu nk...najua wengi wanaelewa nature ya Duka la Jumla
Mapema mwanzoni mwaka jana nikapata wazo la kujiwekea wakiba kwani ""NdoNdo si Chururu"
Nikapata wazo la kujiwekea 27,500 kila siku 27,500[emoji808]365 = 10,037,500 ndani ya mwaka 2017 nikafanikiwa kuweza kupata milion 10 hii ilinipa hamasa na kunipa ujasili mkubwa.
lakini Target yangu kwa mwaka niweze kuingiza 25 milion naomba ushauri wenu wana JF....Ahsanteni