Malawi haina Tume Huru ya Uchaguzi

Hismastersvoice

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2013
Posts
24,608
Reaction score
30,226
Nchi ya Malawi ambayo jana Jumanne 23/06/20 ilifanya uchaguzi wa Taifa baada ya mahakama kutengua ushindi wa Rais ambao ulikuwa na udanganyifu mkubwa, pamoja na kutokuwa na Tume Huru ya Uchaguzi lakini ina Mahakama huru isiyopokea maagizo toka popote, pia ina jeshi la polisi ambalo halijihusishi na uchaguzi na haliegemei upande wowote wa wagombea na vyama vyao.

Matokeo ya awali yanaonesha chama cha Rais aliyefutiwa ushindi wa mwaka jana anashika nafasi ya pili na nafasi ya kwanza inashikwa na aliyekuwa makamu wake.

AZAM TV

Chan. 380, 381 na 382.
 
Sasa ni wazi chaguo la tume wananchi walilikataa na sasa wamelikataa tena.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…