Malawi Airlines, lilifanikiwa kukamilisha safari ya ndege iliyosimamiwa na wanawake pekee

ng'ombo

JF-Expert Member
Dec 1, 2014
418
619
Shirika la ndege la Malawi, Malawi Airlines, lilifanikiwa kukamilisha safari ya ndege iliyosimamiwa na wanawake pekee.

Ndege hiyo ilitua katika uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Marubani na wasaidizi wa abiria kwenye ndege hiyo wote walikuwa wanawake, na ni mara ya kwanza kwa shirika hilo kuandaa safari kama hiyo.

Ndege hiyo ilianza safari yake mjini Blantyre na ilitua kwa muda Lilongwe kabla ya kuja Dar es Salaam.

Shirika hilo la ndege, lilisema lengo la kuandaa safari hiyo ni kufanikisha ulimwengu ambao "unakumbatia jinsia zote".

FB_IMG_1489987390882.jpg

FB_IMG_1489987421004.jpg

FB_IMG_1489987400879.jpg

Source: BBC
 
Mimi binafsi siwezi panda ndege ya hivyo....wakati wa dharura wanawake uwezo wao wa kukontrol mambo ni mdogo.....wanapanick vibaya....and that is natural waulize wataalamu wa saikolojia watakwambia
 
Mkuu unapokata tkt kabla ya kuruka huwezi kujua pilot atakua nani, lakini pia baadhi ya wanawake ni mashujaa tofauti na unavyofikiri, wengine wamediriki hata kuwanyanganya majambazi silaha
 
Safi sana wadada kwa elimu, mmempita mpaka bashite!!??? Bashite wewe kweli bomu.
 
Hawa ndio wanawake wa shoka sio KAMA Wema Sepetu AMBAYE haeleweki hata alichosoma anayepapatikiwa na akina Mbowe na CHADEMA
fb_img_1489987421004-jpg.483640
 
Kule kuna kitu kinaitwa "kioda" wenzetu heshima kwa mabinti ni toka enzi ya president wa muyaya H.K.Banda.Hiyo ilikuwa ngoma ya kina dada tu kumburudisha presida na ilikuwa na maskani Ikulu.
 
Shirika la ndege la Malawi, Malawi Airlines, lilifanikiwa kukamilisha safari ya ndege iliyosimamiwa na wanawake pekee.

Ndege hiyo ilitua katika uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Marubani na wasaidizi wa abiria kwenye ndege hiyo wote walikuwa wanawake, na ni mara ya kwanza kwa shirika hilo kuandaa safari kama hiyo.

Ndege hiyo ilianza safari yake mjini Blantyre na ilitua kwa muda Lilongwe kabla ya kuja Dar es Salaam.

Shirika hilo la ndege, lilisema lengo la kuandaa safari hiyo ni kufanikisha ulimwengu ambao "unakumbatia jinsia zote".

View attachment 483639

View attachment 483640

View attachment 483641

Source: BBC

Na abiria wote walikuwa ni wanawake! Huyo mwenye kijani ni muhabeshi sio Malawi. Malawi hakuna dem mzuri km huyu nakataa katakata
 
Mimi binafsi siwezi panda ndege ya hivyo....wakati wa dharura wanawake uwezo wao wa kukontrol mambo ni mdogo.....wanapanick vibaya....and that is natural waulize wataalamu wa saikolojia watakwambia
Kwa hiyo ukiingia tu ndani ya ndege unauliza jinsia ya rubani?,...Kenya Airways wana mdada mahili ana command Dreamliner yao,one of the best Captain....skills matter not jinsia mkuu..
 
Tanzania tunao pia wadada wanafanya vizuri tu kwenye u pilot ,niwapongeze hawa wa Malawi pia kwa kusimamia kazi yao vizuri ,wanawake wanatuongoza katika kila kitu tusiwa dharau.
 
Mimi binafsi siwezi panda ndege ya hivyo....wakati wa dharura wanawake uwezo wao wa kukontrol mambo ni mdogo.....wanapanick vibaya....and that is natural waulize wataalamu wa saikolojia watakwambia
Ni kweli lakini mafunzo yao yanazingatia jambo hilo pia, ndio maana leseni zao zinatambuliwa kimataifa. Wanawake wanaweza wakiwezeshwa
 
Tanzania tunao pia wadada wanafanya vizuri tu kwenye u pilot ,niwapongeze hawa wa Malawi pia kwa kusimamia kazi yao vizuri ,wanawake wanatuongoza katika kila kitu tusiwa dharau.
Kauli yako yakwanza nimependa jinsi ulivyo mzalendo kwa Tanganyika, salute
 
Back
Top Bottom