Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
Baadhi ya wananchi wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga wamelilalamikia jeshi la polisi wilayani humo kwa vitendo vya unyanyasaji ikiwemo kuwabambikia kesi na kuwaweka rumande bila kuwasajili kwenye kitabu cha kumbukumbu ya washitakiwa hivyo kuwanyima haki ya kisheria katika masuala mbalimbali huku Serikali ikiahidi kuchukua hatua dhidi ya wahusika.
Miongoni mwa wananchi waliofanyiwa vitendo hivyo ni pamoja na Bertha Mabula, mfanyabiashara mjini Kahama ambaye alikumbwa na adha hiyo kwa kubambikiwa kesi na kuwekwa rumande bila kusajiriwa kwenye kitabu cha washtakiwa na baadhi ya askari polisi wa kituo kikuu cha polisi cha wilaya hiyo, ikiwemo vitendo vya unyanyasaji na udhalilishaji.
Kufuatia hali hiyo Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo, ambaye pia ni Mkuu wa wilaya hiyo, Vita kawawa amekili kupokea malalamiko hayo na kuagiza uchunguzi ufanyike na hatua zichukuliwe dhidi ya askari hao huku Jeshi la polisi mkoa wa shinyanga likiahidi kuwawajibisha askari wake watakaobainika kukutwa na makosa.