Malalamiko juu ya Usajili wa Makampuni BRELA

DLN

New Member
Dec 11, 2016
4
2
Waziri wa Viwanda na Biashara, malalamiko dhidi ya Msajili wa Makampuni kutokana na lugha mbaya kwa wateja waendao kusajili kampuni kutoka kwa wafanyakazi.

Moja, utaratibu uliopo ukienda BRELA kusajili kampuni au kulipia ada za mwaka wanakuomba kitambulisho, ukiwapa kitambulisho cha Kura wanakataa hatimaye hufanyiwi kazi na kusababisha serikali kupoteza mapato. Huu utaratbu umeanzishwa na CEO wa sasa.

Kumbuka watu wote wanaokwenda BRELA wanatoka sehemu tofauti kwenye law firm, kwa auditor na kwa watu binafsi. Huyu CEO anapingana na sera ya Rais ya kukusanya kodi.

Pili, kuna mambo mengi yanafanyika hapo. BRELA imekuwa ya wafanyakazi wachache. Ushauri wa wafanyakazi wengine haupo.

Tunaomba Mhe Waziri Mwijage angalia hili suala.

Asante.
 
walipokataa kitambulisho cha mpiga kura walikudai kitambulisho gani?
 
Hilo naungana na wewe ndugu, hata mimi hilo limenikuta na wakakataa kunihudumia. Na sielewi kitambulisho ni cha nini wakati unawapa tu documents wazihakiki kisha wakufanyie assessment ukalipe benk. Hasa yule dada mweupe mnene ndo jipu kabisa, hata Lugha yake kwa wateja sio nzuri
 
Hilo naungana na wewe ndugu, hata mimi hilo limenikuta na wakakataa kunihudumia. Na sielewi kitambulisho ni cha nini wakati unawapa tu documents wazihakiki kisha wakufanyie assessment ukalipe benk. Hasa yule dada mweupe mnene ndo jipu kabisa, hata Lugha yake kwa wateja sio nzuri


MFANO KAMPUNI NDIO NAANZA KUISAJILI KITAMBULISHO CHENYE JINA LA HIYO KAMPUNI NITAKUWA NIMEKIPATAJE WAKATI HAIJASAJILIWA? JE JINA LA KWENYE MEMAT KAMA LIPO SAWA NA LILILOPO KWENYE KITAMBULISHO CHA KURA HUYU DADA KIBONGE KUKATAA KUKUHUDUMIA NI HALALI? NA HIZI LUGHA ZA KEJELI ANAZOTOA HUYU DADA NDIO UTARATIBU MPYA AMBAO BWANA KANYUSI AMEUBUNI? TUNAJUA LENGO NI KUDHIBITI VISHOKA HASA WALE KINA DADA WALIOWEKA KIKUNDI PALE MEZANINE FLOOR NA YULE MLEMAVU AITWAYE TEACHER, PAMOJA NA KUNDI LA KINA NGONYANI, JERRY NA WENGINEO, SISI TUNAUNGA MKONO ,BASI ZITAFUTWE NJIA SAHIHI KULIKO HII MLIYOBUNI, NI MUHIMU HATUA ZA HARAKA ZICHUKULIWE KUREKEBISHA HALI HII HASWA LUGHA ZA HUYO DADA
 
BRELA wapo vizuri ukiwa upo na full required documents,nimesajili kampuni hapo km mwezi mmoja uliopita wanapiga kazi sana aiseee,km ni mapungufu ni madogomadogo sana
 
Back
Top Bottom