JAMHURI
JF-Expert Member
- Dec 15, 2010
- 449
- 60
Zikiwa zimebakia siku tatu wananchi kuingia kwenye chumba cha kufanya maamuzi ya nani aongoze kwa kupiga kura, hii leo hapa Wilayani Kiteto lile dili la kisiasa kwa viongozi wa mila Malaigwanani wa jamii ya kifugaji maasai, kutaka kupata fedha kupitia siasa limebainika baada ya kujikuta hawana mwelekeo na kuwafanya jamii hiyo kutanga wasijue wakumchagua.
Wagombea watatu wa ngazi ya Ubunge akiwemo wa CCM Emanuel Papian, CHADEMA Kidawa Othaman, na CUF Hasani Losioki wamekuwa wakihaha juu ya jamii hiyo iliyodaiwa kutishia kutompa kura mgombea asiyekubalika na mwenye maslahi kwao.
Baada ya kuhaha kwa muda mrefu huku wakila fedha za wagombea hao sasa wamebakia njia panda baada ya kukosa mwelekeo wa nani wawaelekeze wafuasi wao kuwa ndiye atakayelinda maslahi yao ya kifugaji.
Maslahi hayo ni yale ya kulinda maeneo ya malisho ambayo yamekuwa na changamoto kubwa kwao na kusababisha mgogoro wa wakulima na wafugaji
CCM, CHADEMA, CUF wote wanatumainia hatma ya jamii hiyo wanaotamba kuwa wako wengi kuliko makabila mengine hapo wilayani Kiteto.
Hali bado sio shwaari, hakuna anayejua nani ni nani.