makutupora
JF-Expert Member
- Jul 7, 2015
- 2,482
- 5,133
Mwenzenu Makutupora nimekuja kutoa shukurani!
Mwenzangu, wanajukwaa wenzangu!
Najua imepita muda tangu nitume ombi langu la msaada, lakini ninachoamini ni hiki: Asiyeweza kuwa mwingi wa shukurani ni mtu mbaya sana!
Kwanza kabisa, naomba kutoa shukrani za dhati kwa kila mmoja wenu mlionitafuta kwa PM, mlioonyesha nia ya kunisaidia — kwa namna moja ama nyingine, hata kama hatukufikia muafaka, bado ninyi ni watu wa kipekee sana kwangu. Moyo wangu unawashukuru sana!
Wale wote tuliowahi kuongea kwa simu, au hata kwa kuchat kawaida — naomba moyo wangu wa shukurani uwafikie pia!
Mmeonyesha upendo na kujali zaidi ya maneno.
Shukurani za pekee na za kipekee kabisa naomba zifike kwa Shangazi Mambo — mbali na mada zako za kufurahisha watu, hujawahi kuniacha, umebaki kuwa Malkia wa nguvu kwangu. Mungu pekee ndiye anayejua hili.
Kwa Rais wa Majobless, Balotola, na wengine wote ambao kwangu mmekuwa kama ndugu, japo hata sura zenu sizijui — nawashukuru sana sana.
Nimekuja hapa kutoa shukurani kwenu nyote mliojali maumivu yangu. Kikubwa zaidi ni kwamba, nimepata kazi ya kujitolea hapa Mwanza — nimeanza na hadi sasa nimefikisha wiki moja!
Walionipa kazi wamenipatia malazi na chakula cha mchana. Ni taasisi nzuri yenye ushirikiano mkubwa sana. Leo hii ndio nimepewa barua rasmi ya kutambulika kama mfanyakazi tarajiwa, lakini wameshanisaidia mambo mengi sana.
Nina amani, furaha, na muda wa kuomba na kumuabudu Mungu. Napata muda wa kufuatilia ibada za Koinonia. Kubwa zaidi, Mama pia anaendelea vizuri — jambo ambalo kwangu ni faraja kubwa mno.
Kwa hakika sitaki kuongea mengi, ila nimekuja kutoa shukurani zangu za kweli. Sijui ni nani aliwahi kuongelea ule wimbo wa Lucky Dube - “Usizi” — ila ndiyo wimbo ninaousikiliza hata sasa… nausikiliza kila muda.
Katika yote, poleni shukurani zangu!
Mungu awabariki sana — Mlikuwa nami kwenye giza, na sasa mnashuhudia nuru!
Makutupora!
Samaleko.
Soma Pia: Shida haina hodi, mwenzenu nimefika mwisho, naombeni msaada