Makusudio chanya na Biashara yako

MtotoWaMzeeWaSiku

New Member
Jan 2, 2017
3
2
Mafanikio kibiashara utegemea hatua za kimasudi
Na frank kadidi/MtotoWaMzeeWaSiku

Mtu awekapo dhamiri ya kujiingiza katika shughuli fulani akiwa na maazimio kuwa kupitia jambo hilo unafuu wake utapatikana uweka matumaini na imani kuwa sasa anakwenda kuachana na hali fulani aliyokuwa nayo hapo awali na sababu ya shauku,hamu pamoja na hamasa anayokuwa nayo kwa wakati huu upelekea kwa namna moja kusahau kuzingatia njia bora zitakazo mvusha na kumpeleka katika hatua nyingine anayoitazamia.

Katika jamii yetu ya kitanzania wengi wetu uwa tuna amua kufanya baadhi ya mambo ili tu kupata afadhari ya maisha yetu hii utokana na kutazama namna wengine walivyo au wanavyofanikiwa kupitia mambo hayo tunasahau kwamba hata kwao pia haikuwa na urahisi wa kufikia hapo walipofika kwa wakati uwatazamapo nahi ndio sababu kubwa yakufanya wengi wetu kushindwa kustahimili changamoto tunazo kumbana nazo katika shughuli tunazofanya kupitia mitazamo ya watu wengine.

Turejee hapa katika mtazamo wa kibiashara ukiingia katika biashara yoyote pasipo tathimini yakinifu sio rahisi kupata mrejesho ulio mzuri haijarishi utatumia nguvu kiasi gani…inachotakiwa ni hatua za kimasudi katika kufanikisha kile upangacho kufanya kwa wakati.

Ili kuweza kuiona biashara yako ikisonga vyema unatakiwa kukusudia kuifanya kwa namna tofauti na vile ambavyo wengine wamekuwa wakiifanya Mfano:wewe umeamua kufanya biashara ya kuuza chakula na katika mtaa huo kuna watu wengine zaidi ya wawili nao ufanya biashara iyoiyo ili kuweza kupata upekee wa biashara yako unatakiwa kuwa na makusudio ya tofauti navile ambavyo wenzako wamekuwa nayo katika bishara zao,vipo vitu uwezavyo kubadilisha kimtazamo (mabadiliko katika sehemu yako ya biashara) na vingine katika utendaji.

Kwasababu utakuwa umeamua kufanya vitu vya tofauti na kuchukua hatua kwa namna ya kipee watakiwa kukumbuka kuwa hapa hakuna mtu utakaye kuwa ukimwangilia ili kupata mwongozo wa namana ya kufanya shughuli zako zaidi ya kuamini uwezo wako na kushirikisha mawazo yako wewe mwenyewe (ubunifu wako) jambo la kuzingatia ikiwa utajisahau ni rahisi kupoteza uelekeo

Uwekapo utofauti katika icho ufanyacho kitu icho ugeuka kuwa alama ya kukutambulisha wewe na biashara yako.
 
Back
Top Bottom