WanaJf ,
Ni miaka miwili tu imesalia kuelekea kwenye uchaguzi mkuu panapo mwaka 2015, ni suala la wazi kabisa lisilopingika kuwa umaarufu na ungwaji mkono toka kwa wananchi kwa chama cha CCM umekuwa ukishuka kadiri siku zinavyokwenda huku vyama pinzani hususani CHADEMA kimeendelea kuungwa mkono siku hadi siku na hivyo kuonyesha matumaini makubwa ya kuibuka na ushindi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Pamoja na hayo yote kuna makundi ambyo ni muhimu sana endapo wataamua hakika CCM haina ujaja lazima itang'oka, makundi haya ni kama ifutavyo:
1. Kundi la Wasomi
Kwa hali ilivyo sasa katika siasa za Tanzania asilimia kubwa ya wasomi hawakubaliani kabisa na utawala wa CCM wengi wanauunga mkono upinzani ila tatizo kubwa ni moja kuwa wengi wao hawajajitokeza moja kwa moja kuwa mstari wa mbele kwenye mapambano ya wazi, wameendelea kuikataa CCM kwa chini chini hususani wale walioajiriwa na serikali.
Hili kundi naliona ni muhimu sana kwa mabadiliko endapo litaamua kweli kweli.
2. Kundi la wapenda mabadiliko ambalo kwa muda mrefu limekwisha kata tamaa
Hawa si wengine, ni wale watu wote ambao siku nyingi wamekuwa na kiu ya kuona mabadiliko yakitokea lakini imekuwa kinyume na matarajio yao. Hili kundi lina umuhimu mkubwa na ndo wale watu wote ambao hawajitokezi kupiga kura kwa kukata tamaa kuwa hata tukipigia upinzani tunajua CCM itashinda tu, si kana kwamba wanaipenda CCM ila hawaamini kama Tume ya Uchaguzi inaweza kutenda haki.
Ili linathibitishwa na watu wengi kujiandikisha lakini hawaendi kupiga kura, kwa uchunguzi nilioufanya wale wote wanachama hai wa ccm na wafuasi ni waaminifu sana kwenda kupiga kura na hapo ndipo ushindi wa ccm unapopatikana, wanajitokeza wachache kupiga kura kati ya wengi waliojiandikisha na wengi katika hao wachache ni wana ccm
3. Kundi la vijana ambalo ndio lenye matamanio makubwa ya mabadiliko
Ni wazi kuwa hawa ndio wenye nchi haswa, hii ni kutokana kuwa kwa kila uongozi mbaya utakao kuwepo madarakani yeye kijana ndiye atakayeathirika zaidi kuliko ambao ni watu wa umri mkubwa (wazee) . Katika maamuzi na mabadiliko naliona kundi hili kuwa muhimu na kutafakari sana juu ya mstakabali wa Taifa hili, hawa kwa kifupi ndiyo wenye nchi.
Kundi hili likiamua kuweka uzalendo mbele kuliko kuwa na maslahi binafsi yanayohusisha itikadi za kichama, kidini, kikanda zisizokuwa na msingi wowote hakika Tanzania tunayoitaka tunaenda kuiona muda sio mrefu ujao. sioni sababu sana kwa vijana kutawaliwa na unafiki wa itikadi kuliko kuongozwa na haki na uzalendo
Wito kwa vijana tupongeze panapostahili kupongeza na tukosoe bila uoga panapositahili kukosolewa bila kujali itikadi zetu maana hizo hazitatusaidia badala yake tutakuwa tunaliangamiza taifa
Kwa kumalizia ni wazi kuwa viongozi wetu waliotangulia wametambua umuhimu wa vijana katika taifa hili, nilibahatika kumsikiliza Mh. Waziri Mstaafu Mzee Malecela kwenye kipindi cha DK 45 ITV, akasema "Taifa hili lina rasilimali nyingi mno, lakini tumefika hapa tulipo kwa sababu tumekuwa na tatizo la muda mrefu katika mikataba na wawekezaji, hatujui kuiangalia mikataba labda vijana wetu hawa watatusaidia kwa sasa" katika hili nilimuunga mkono 100% lakini pia binafsi natambua kwamba ili taifa liende vizuri na mambo yasijeyakaharibika linahitaji waliotangulia na wenye uzoefu (wazee)
Nawasilisha