Makumi ya wanamgambo wauawa katika mapigano Uturi Congo

STRUGGLE MAN

JF-Expert Member
May 31, 2018
8,638
16,566
Makumi ya wanamgambo wauawa katika mapigano Ituri, Kongo DR


Wanamgambo 23 wameuawa katika mapigano baina yao na Jeshi la Ulinzi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (FARDC) katika mkoa wa Ituri, kaskazini mwa nchi.

Hayo yalisemwa jana Ijumaa na msemaji wa jeshi Luteni Jules Ngongo katika mkutano na waandishi wa habari ambapo ameongeza kuwa, baada ya kujiri makabiliano makali baina askari usalama na wanamgambo wa CODECO siku ya Alkhamisi, jeshi la nchi hiyo limefanikiwa tena kudhibiti vijiji vinne vilivyokuwa mikononi mwa wanamgambo hao, yapata kilomita 90 kaskazini mwa Bunia, katika eneo la Djugu.

Luteni Ngongo amesema, "wanamgambo 23 wameuawa, wengine 12 wametiwa mbaroni, na bunduki saba za AK 47 zimepatikana katika operesheni hiyo."


Hii ni katika hali ambayo, mwishoni mwa mwezi uliopita wa Aprili, watu 43 waliuawa katika siku tatu za makabiliano baina ya wanajeshi na magenge ya wabeba silaha mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Eneo la mashariki mwa DRC limekuwa likishuhudia machafuko ya mara kwa mara baina ya makundi ya wanamgambo kwa upande mmoja na wanamgambo na maafisa usalama kwa upande mwingine, kutokana na kuwa na utajiri mkubwa wa madini hususan dhahabu na almasi.





4bn0cddee2d08auhos_800C450.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom