Maktaba: Mh. Mwenyekiti Freeman A. Mbowe, 1999

Tangopori

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2012
Posts
1,628
Reaction score
1,290


Ndugu Freeman Aikaeli Mbowe (sasa Mbunge wa Hai na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo) akikabidhi zawadi kwa Hoyce Temu, ambaye alishinda taji la Miss Tanzania mwaka 1999 kwenye ukumbi wa Club Billicanas jijini Dar es Salaam. Kwa sasa Hoyce Temu ni mtayarishaji na mtangazaji wa Kipindi cha Mimi na Tanzania kinachorushwa na Channel Ten, mwandishi wa makala katika gazeti la The Citizen na mfanyakazi katika Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Ofisi ya Tanzania.
 
Nimeipenda simu ya muheshimiwa.

Enzi zile ilikuwa lazima uiweke sehemu ya wazi watu wajue una simu.
 
Nokia ile yenye upembe mrefu anafu ilikuwa ikiwaka taa ndio ya kwanza mimi kumiliki
Nilikuwa lazima nichomekee na niichome kila mtu aone
 


Duh watu wametoka mbali kila nikitazama hiyo simu najikuta nacheka mwenyewe haaa haaa niliwahi kuchukua kipusa cha ukweli kwasababu ya simu aise siyo siku hizi hata wauza karanga wanamiliki simu wakati huo ilikuw shedaaa .
 


Mwenyekiti wa Maisha CHADEMA na Mbunge wa Hai akimkabidhi Zawadi mshindi wa Miss Tanzania Hoyce Temu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…