Makoti ya Android: HTC Sense

ManiTek TV

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2011
Posts
410
Reaction score
159
​
Katika sehemu hii ya pili tutazungumzia koti linalovalishwa kwenye Android ambayo hutolewa na kutumika kwenye simu za High Technology Computers (HTC). Toleo jipya kabisa ni lile lililotumika kwenye simu yao mpya yaani HTC One, toleo hili hujulikana kama Sense 5.0, HTC ilikuwa miongoni mwa kampuni za mwanzo kutoa koti la Android, HTC walichukua uzoefu wao wa kutumia HTC Sense kwenye simu za Windows Mobile (WM) kabla Microsoft kuanza kutoa Windows Phone, sense ya WM iliwapa HTC umaarufu mkubwa na mauzo mazuri miaka ya nyuma.

Kwa mujibu wa mtandao wa HTC, Miongoni mwa matumizi ya kipekee kwenye Sense 5.0 ni kule kuzima sauti kwa kuifunika simu, yaani kuiweka mahala huku skrini ikiwa imeelekea chini, hivyo kama simu inaita hunyamaza (silence). Matumizi haya pia yalikuwepo kwenye simu za HTC zilizotangulia zlizotumia Sense 4.0 kwenda mbele. Vile vile kwa kuigeuza simu wakati tayari umeanza kuongea Sense 5.0 hukuwezesha kuwasha na kusikiliza maongezi kwa spika (speaker phone) badala ya kuweka sikioni. Spika ya HTC One iko nyuma ya simu.

Pia HTC katika Sense wameibadili smart dial wa kawaida, kama tunavyoelewa kwenye Smart Dial ya Android kama una namba umeihifadhi kwa jina la Gajetek Habari ili kuipata namba hiyo inabidi uanze kuandika Gaje ndio ije namba. Kwenye HTC unaweza tu kuandika GH badala ya Gajetek Habari na namba ikaja wenyewe. Vile vile ukiwa kwenye orodha ya majina na namba ulizohifadhi unapogusa kwa vidole viwili na kupeleka juu au chini Sense inakuruhusu kuruka kwa mpangilio wa herufi badala ya kwenda jina moja baada ya jengine.

Kwa upande wa kibodi, Sense inakupa za aina tatu, Super size kwa wale wenye matatizo ya macho ambapo hukupa miandishi mikubwa mno, trace keyboard kwa wale wenye kuweza kutumia utaalamu wa swipe katika kuandika na Dyanamic keyboard kwa ajili ya kubadili kirahisi kati ya herufi na namba.
​
Browser nayo imewekewa mikogo kadhaa tofauti katika Sense, pure reading mode ni aina ya kwanza ya mikogo hiyo, hii huondoa picha, matangazo ya biashara na ghasia zote kwenye kurasa na kukupa maandishi safi yenye mpangilio mzuri. Kwa kifupi pure reading mode ni sawa na reader ya browser ya Safari inayotolewa na Apple. Pia browser ya HTC ina incognito na instant tabs zilizopangiliwa katika mtingo wa maboksi.

Kwa upande wa picha Sense imetoka na Zoe. Hii hukuruhusu kupiga picha ambazo zinakuwa na uhai fulani hivi, yaani picha hizi kama mtu amepepesa macho basi unapoiangalia huonyesha anavyofunga macho, inakuwa kama kivideo kifupi cha sekunde tatu bila ya sauti. Hivyo unapata mitikisiko na mambo kama hayo.

HTC pia wameiongezea Sense kitu walichokiita HTC Blink Feed. Hii inapatikana kwenye "Home Screen" ambapo hukusanya habari zote za mitandao ya kijamii unazozipokea mahala pamoja, hivyo Google+, Twiiter, Facebook na Pinterest zote utazipata Blink Feed badala ya kufungua apps nne tofauti kuangalia maoni (comment and feeds) mapya. Pia ina muonekano na namna ya kutumia ya kuvutia mno.

Usikose sehemu ya tatu ya makala hii tutakapozungumzia TouchWiz ambalo ni koti la simu za Samsung, tutaongelea mambo kadhaa ya simu mpya ya Samsung Galaxy S4.

Chanzo:
Gajetek - Gajet na Teknolojia: Makoti ya Android: HTC Sense
​
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…