Makosa ya Kimtandao: Mtoto wa Chacha Wangwe afikishwa Mahakamani Kisutu

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,739
32,866
image.jpeg

BOB Chacha Wangwe (24), mtoto wa mwanasiasa marehemu Chacha Wangwe, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa tuhuma za kuchapisha taarifa za uongo katika mitandao ya kijamii, anaandika Faki Sosi.

Akisoma kesi hiyo namba 167, Paul Kagoshi mbele ya Waliarandwe Rema, Hakimu Mkazi katika mahakama hiyo amesema kuwa, Bob Chacha Wangwe amefikishwa mahakamani hapo kwa kutenda kosa la kuchapisha taarifa za kupotosha katika ukurasa wake Facebook.

Mshitakiwa anadaiwa kutenda hayo tarehe 15 Machi na kwamba alichapicha maneno haya “Tanzania ni ambayo….inajaza chuki wananchi … matokeo ya kubaka Demokrasia Zanzibar ni hatari zaidi ya muungano wenyewe…. Haiwezekani nchi ya Zanzibar kuwa koloni la Tanzania bara kwa sababu za kijinga.

Mtuhumiwa amekiri kutenda makosa hayo hivyo amerudishwa rumande baada ya kukosa dhamana. Kesi hiyo itatajwa tena tarehe 17 Mei mwaka huu.
 
Mshitakiwa anadaiwa kutenda hayo tarehe 15 Machi na kwamba alichapicha maneno haya “Tanzania ni ambayo….inajaza chuki wananchi … matokeo ya kubaka Demokrasia Zanzibar ni hatari zaidi ya muungano wenyewe…. Haiwezekani nchi ya Zanzibar kuwa koloni la Tanzania bara kwa sababu za kijinga.”

Huyu naye pilipili shamba yamwashia nini?
Swala la uchaguzi wa Zanzibar si swala la muungano kwa mujibu wa katiba ya muungano wa Tanzania.Anashobokea vitu vya nchi ingine isiyomhusu AMBAKO YEYE SI MPIGA KURA na haruhusiwi na si raia wa kule.

Wazanzibari wenyewe wako kimya yeye anashobokea.Ona sasa yanayomkuta.
 
Je, ni kweli kakiri kosa au kakubali kosa? Maana ukikiri kosa huwa inafuata hukumu tu na huwa mtuhumiwa anapata mda mchache wa kujifikiria kisha kusomewa shitaka tena na akiendelea kukiri hukumu hufuata.

Huenda umesikia akikubali kosa. Hapa huwa kunabaadhi ya mambo mtuhumiwa huwa hakubali na hayo ndio huwa hoja za kubishaniwa mahakamani. Hivyo tusaidie kwa hilo.

Huyu kijana inasemekana ni mweledi wa sheria hivyo huenda kaona hicho alichokifanya kitampa kick kwa umma siunajua mwaka 2020 si mbali sana.
 
Huyu naye pilipili shamba yamwashia nini?
Swala la uchaguzi wa Zanzibar si swala la muungano kwa mujibu wa katiba ya muungano wa Tanzania.Anashobokea vitu vya nchi ingine isiyomhusu AMBAKO YEYE SI MPIGA KURA na haruhusiwi na si raia wa kule.

Wazanzibari wenyewe wako kimya yeye anashobokea.Ona sasa yanayomkuta.
Aachane na mambo ya NCHI ya watu
 
Huyu naye pilipili shamba yamwashia nini?
Swala la uchaguzi wa Zanzibar si swala la muungano kwa mujibu wa katiba ya muungano wa Tanzania.Anashobokea vitu vya nchi ingine isiyomhusu AMBAKO YEYE SI MPIGA KURA na haruhusiwi na si raia wa kule.

Wazanzibari wenyewe wako kimya yeye anashobokea.Ona sasa yanayomkuta.
Acha woga kufa kiume utoweke basi!
 
Je ni kweli kakiri kosa au kakubali kosa? Maana ukikiri kosa huwa inafuata hukumu tu na huwa mtuhumiwa anapata mda mchache wa kujifikiria kisha kusomewa shitaka tena na akiendelea kukiri hukumu hufuata.
Huenda umesikia akikubali kosa. Hapa huwa kunabaadhi ya mambo mtuhumiwa huwa hakubali na hayo ndio huwa hoja za kubishaniwa mahakamani. Hivyo tusaidie kwa hilo.
Huyu kijana inasemekana ni mweledi wa sheria hivyo huenda kaona hicho alichokifanya kitampa kick kwa umma siunajua mwaka 2020 si mbali sana.

Hili suala litakuwa kubwa tofauti na watu wanavyolichukulia, maana raisi alisema znz haimuhusu na matatizo yao hayamuhusu
 
Huyu naye pilipili shamba yamwashia nini?
Swala la uchaguzi wa Zanzibar si swala la muungano kwa mujibu wa katiba ya muungano wa Tanzania.Anashobokea vitu vya nchi ingine isiyomhusu AMBAKO YEYE SI MPIGA KURA na haruhusiwi na si raia wa kule.

Wazanzibari wenyewe wako kimya yeye anashobokea.Ona sasa yanayomkuta.
Not true!kilichofanyika zanzibar alivyosema wangwe ni sahihi kabisa acha wafu wazike wafu wao its pain kusema tz ni nchi ya kidemocrasia pesa za mcc zimezuiwa kwasababu ya uchaguzi wa zenji acha kuleta uccm wako hapa simama kwenye hoja.
 
Kila siku tunawaambia hamieni jamii forum hawasikii, unaona sasa, jamii forum wakiona umeposti kitu ambacho kitakuingiza mwanachama wao kwenye matatizo au umeposti utumbo wanadelete haraka sana, Facebook ukiposti chochote kile wanakiacha kama sticky ili ukamuliwe utifi.
 
Back
Top Bottom