Historia ya Mikasa ya Zanzibar haiwezi kutenganishwa na wahafidhina wa CCM kule Zanzibar walau tokea kuja kwa mfumo wa vyama vingi mwanzoni mwa miaka ya 1990. Kwa bahati mbaya kila migogoro iliyohusishwa na chaguzi na migogoro ya kisiasa kule Zanzibar haikuicha salama Tanzania ingawa IMEPITA KWA HATUA TOFAUTI. Ndio hivyo hata viongozi wa JMT kuanzia Mzee Mkapa, kikweete na sasa magufuli wote wamekutana na zahma hiyo.
Rejea matukio ya chaguzi na malamiko yote ya uharibifu wa demokrasia kuanzia uandikishaji hewa, utumizi usio halali wa vikosi, tume ya uchaguzi, hilba za chaguzi na matukio ya utesaji ambayo mara zote hulalamikiwa na wadau wa siasa na asasi za haki za binadamu hunasibishwa na utawala wa CCm Zanzibar kushindwa kuchukuwa hatua na kunasibishwa na uhafidhina wa kungangania madaraka. Habari ni ndefu sana.
Leo tuangalie kile kinachoendelea kumtesa Rais magufuli baada ya kilichotokea Zanzibar, mwaka 2015. Tatizo ni lile lile la uhafidhina wa kutokubali demokrasia. Na imekuwa ni desturi uongozi wa JMT kuwaunga mkono wahafidhina hata kama wanahatarisha maslahi ya nchi nzima. Baada ya kufutwa uchaguzi wa 2015 ambao bila ya shaka vyombo vya dola vya JMT vilihusishwa, vimeiingiza Serikali ya rais Magufuli katika fadhaa ya kukosa uungwaji mkono wa misaada na nchi za magharibi jambo ambalo wataalamu wanasema limechangiwa zaidi na kukatishwa misaada hiyo na limetikisa mipango ya nchi na kuzidisha umasikini kwa watanzania. Ingawa awamu ya tano haitaki kukiri hilo ukweli huo uko wazi.
MAKOSA YA CCM ZANZIBAR.
Kutoheshimu maamuzi ya wengi na kuvuruga demokrasia na dhana ya kuwa hawawezi kuingiliwa na yeyote huku wakifaidi uungwaji mkono na jamuhuri. Makosa haya yameigharimu nchi tokea 1995 hadi sasa kwa Tanzania kuharibu taswira yake kimataifa, kuzalisha wakimbizi, kutokea mauaji, kuzuiwa misaada na kuzuka mitafaruku ya kijamii hasa kule Zanzibar.
Bado rais Magufuli anajipa matumaini ya kuweza kupita salama na hatimae hatuoni na hatujui anaipeleka wapi nchi. Uchumi hauko sawa, huduma zimesinyaa na mianya ya ajira imejificha, Wazungu bado wameshikilia msimamo wa kuheshimiwa maamuzi ya 2015, wahafidhina na wao wamegoma kukubali hadi sasa.
CCM Zanzibar inadekezwa, imelewa deko hilo la JMT haya ni miongoni mwa makosa.
WALIPOSAHAU CCM NA RAIS MAGUFULI.
Wamesahau kuwa huwezi kupambana na mabadiliko, unaweza tu kuchelewesha mabadiliko.
Hakukuwa na sababu kwa CCM kugoma kukubali mabadiliko ya uongozi kwa kuwa wameshindwa tu na hatimae kuingiza nchi katika mtafaruku. Walisahau kuwa Zanzibar ilishachaguwa mabadiliko tokea 1995,2000,2005 na 2010. Wamesahau kuwa Zanzibar ilikubali kuongozwa kwa GNU iliyopo katika Katiba yao, wamesahau kuwa juhudi za dunia zilikubali Zanzibar iendeshwe kwa ushirikiano wa vyama vyenye kuungwa mkono na wazanzibari wengi. Hili kosa la kurejesha mambo ya kabla ya 2010 kulirejea tena mwaka 2015 amini maneno yangu litaigharimu CCM yote, Tanzania na watanzania. Kosa lile la KUDEKEZWA limewasahaulisha tena kuwa LAZIMA mgogoro wa Zanzibar upatiwe dawa mujarabu.
Ikiwa dawa ya GNU ambayo ilidumu kwa miaka 5 tu haikuendelezwa na CCM wakidhani utawala wao ndio utadumu jee wanajuwa dunia itakuja na njia gani nyengine ? hili suali wangelazimika kujiuliza CCM na rais magufuli kabla ya kutumia nguvu kulazimisha marejeo ya uchaguzi wa 2016. Wamesahau yote haya kwa mshindo wa DEKO na UHAFIDHINA.
MAKOSA YA RAIS MAGUFULI.
Kufanya makosa yale yale ya kiufundi ya KUDEKEZA na imani kwamba anaweza kushindana na DUNIA. Wenzake akina mkapa na kikwete walikuja na MIAFAKA FEKI, yeye amekuja na vitisho na ukaidi. Dunia inakwenda kwa principles. Ikiwa huu ni mwaka karibu wa pili JPM haoneshi dalili za kufanya japo usanii wa kuzuga walau kufanana na ule wa Kikwete wa GNU na ule wa muafaka wa mkapa. Anadhani labda DUNIA HAIMUONI NA ANAFIKIRI LABDA DUNIA IKO KIMYA.
Tukumbuke kuwa Walioasisi mpaka kupatikana kwa GNU walipata baraka za wakuu wa dunia na ni imani yangu kuwa huo ndio msimamo wa dunia kwa maslahi ya wakuu wa dunia. Kujiitia imani kuwa haya yatapita ni kudharau matatizo ambayo jitihada za wakubwa wa kidunia na fedha zao ndio zimeleta nafuu kwa kuja GNU leo tena nchi irudi kwenye mitafaruku kwa sababu tu ya kulindwa CCM hivi haya yatapita bure? mimi nadhani hapana, ni suala la muda tu.
MWELEKEO.
Kuna tetesi nyingi za anayoyafanya rais magufuli na awamu yake ya tano kuwa yuko katikati ya mapambano na wamagharibi ambao wameleta masindikizo ya suala la Zanzibar. Wakati hajafanyia kazi mapendekezo yeye yuko katika kukwaruzana akiamini watalegeza msimamo.
Kama ni kweli basi njia hiyo haifai. Tanzania kama nchi changa inatakiwa itumie njia za kidiplomasia kufikia malengo yake.
Rais magufuli, ufumbuzi wa suala la Zanzibar hautapatikana kwa jazba na hadaa na ni imani yangu kuwa unajuwajuwa waliolikwamisha suala hili.
Tathmini yangu kuhusu hili la wahafidhina wa CCM Zanzibar na sokomoko la demokrasia, jiandae kupokea masindikizo ya Zanzibar huru na kuvunjika kwa Muungano au kuheshimu maamuzi ya demokrasia na kuulinda muungano wetu. Huu si utabiri bali tathmini yangu
mimi mlalahoi. Usiniulize sindikizo hilo litatoka wapi lakini kumbuka neno moja tu WAKATI.
Kishada.