Stabilaiza
JF-Expert Member
- Jul 11, 2012
- 1,843
- 1,143
Na hapa ieleweke wazi tangu mwanzo kuwa nchi hii ni ya kila mwananchi na katiba ya Jamuhuri ya muungano inatoa fursa ya mwananchi kushiriki katika maendeleo ya nchi yetu ikiwemo kuchagua viongozi, kusifia au kukosoa. Makosa ya serikali ya Magufuli ni kuwawaumini wa nadharia zisizokuwa sahihi katika kuongoza, lakini kwa serikali hii niseme tu kwamba si kuongoza bali kutawala. Makosa hayo ni kama ifuatavyo:
(a) Kuamini katika maendeleo ya vitu badala ya maendeleo ya watu
Msingi wa nadharia hii ni ubepari kutoka nchi za magharibi ambapo thamani ya mtu hupimwa kwa vitu anavyomilki. Serikali ya awamu ya tano imejikita katika kuleta maendeleo ya vitu huku wakisahau maendeleo ya watu. Kubomoa nyumba za watu, ambapo kwa kweli ni kuleta maafa na kuwaacha waathirika hawa wa maafa bila kuwaandalia msingi wa maisha yao si kuleta maendeleo. Huwezi kuleta maendeleo huku unawaacha watu bila makazi. Watoto wadogo, akina mama wajawazito, walemavu, wazee wote wanaachwa tu. Ukweli ni kuwa hakuna maendeleo ya vitu bila maendeleo ya watu. Suala lingune ni serikali ya Magufuli kutaka kufunga fikra za watu. Unaletaje maendeleo halafu watu wanataka kuondolewa uhuru wa msingi wa kuzaliwa wa kufikiri na kutoa mawazo?. Kwa mfano Dr. Mahanga ambaye nilimdhania kuwa ni boga- hasa pale alipotaka kulazimisha ushindi katika serikali za mitaa, ametumia haki yake ya kuzaliwa na ya kikatiba kufikiri na kuchambua vizuri sana ukubwa wa serikali ya Magufuli. Ulikuwa ni uchambuzi lakini anatishwa kwamba hakutakiwa kuchambua. Kwa hiyo watu waiachie serikali ifikiri kwa niaba yao? Nani kasema hili linawezekana?. Hakuna maendeleo ya vitu bila maendeleo ya watu. Malazi pamoja na uhuru wa kufikiri na kutoa mawazo ni sehemu ya maendeleo.
(b) Kuamini kuwa serikali ndiyo yenye haki ya kuwawajibisha wananchi
Mfano wa bomoa bomoa bila hata kufikiria mara mbili kuwa watu hawa walijenga sehemu walizojenga serikali ikiwepo. Tena serikali imekuwa ikikusanya kodi kutoka kwenye nyumba zinazobolewa. Serikali ya CCM haifikirii kwamba inatakiwa pia kubeba lawama katika hili kwa sababu ujenzi huo umesababishwa pia na watendaji wa serikali. Serikali haitaki kuwajibika na badala yake inajiweka pembeni na kuwaona wananchi peke yao kuwa wakosaji wanaotakiwa kuwajibika kwa serikali lakini yenyewe haitaki kuwajibika kwa wananchi waliowachagua kwa kuwasikiliza. Uwajibikaj ni wa pande mbili, si wa uoande mmoja. Hili serikali ya sasa inaonekana kutolijua au inalipuuza.
(c) Kutokuwa na huruma kwa binadamu wenzao
Nafikiri serikali ya awamu ya tano inawatu wenye huruka ya kufurahia watu wengine wanapopata matatizo. Kama viongozi wetu wangekuwa wanahuruma ya empathy kwa kuvaa viatu vya watu wengine hakika wasingeweza kusababisha maafa. Walitakiwa watambue kuwa hawa watu hata kama wamekosea ni binadamu wanastahili kuishi. Bomoa bomoa ya serikali ya CCM ni maafa makubwa kwa wananchi. Na kama yalivyo maafa mengine, serikali ilitakiwa kuwasaidia watu hawa ambao serikali imewasababishia maafa. Lakini wapi, hakuna huruma.