Viongozi wetu wa sasa ni wakubwa kama tembo! Walipotaka kumjengea nyumba kubwa pale Butiama, Mwalimu alishikwa na mshangao kwa nini ajengewe jumba hilo, kwani yeye hafikii ukubwa wa tembo. Ukitokea muujiza wa Mungu Mwalimu akafufuka na kuziona nyumba waishizo viongozi wetu sasa, hakika atashangaa na kufa kwa msituko wa moyo!