MakongoroMahanga alikuwa anasubiri kesi iishe au uteuzi ndio aendelee na ujenzi wa nyumba yake

Livanga

JF-Expert Member
Apr 15, 2010
469
148
Baada ya kimya cha muda sasa tunaona mafundi wamerudi kazini kwenye ujenzi wa jumba lake maeneo fulani jijini dar. Je alikuwa anasubiri kuona kama bado amebaki kwenye baraza la walaji ndio aendelee ama alikuwa anasubiri kesi. hii inadhirisha kuwa bado kunyonywa kuko palepale.
 
ni bora kuwa muwazi na unachokiandika taja jumba lake liko wapi na ni muda gani kazi ilikuwa imesimama
 
jumba liko mikocheni migombani street karibu na repoa inasemekana kiwanja kilikuwa cha BOT yeye alipotia timu akapiga chini jengo akaotesha lakwake kama linavyoonekana hapo chini. nilishindwa kuweka picha mida coz sikupita pale asubuhi IMG_0255.JPG IMG_0254.JPG
 
Viongozi wetu wa sasa ni wakubwa kama tembo! Walipotaka kumjengea nyumba kubwa pale Butiama, Mwalimu alishikwa na mshangao kwa nini ajengewe jumba hilo, kwani yeye hafikii ukubwa wa tembo. Ukitokea muujiza wa Mungu Mwalimu akafufuka na kuziona nyumba waishizo viongozi wetu sasa, hakika atashangaa na kufa kwa msituko wa moyo!
 
Kutoka uongozi ni dhamana hadi uongozi ni utwana

Yaani ambacho siwaelewi watz aka wadanganyika,hivi sasa mtu akiwa kiongozi tu hamtaki hata awe na maendeleo! Sasa Mahanga nae amewaibia nini? Muwe wazi hapa, vinginevyo tutahesabu ni wivu na majungu!
 
Mkuu kuna tatizo gani hapo mbona Slaa nae anajenga jumba lake Kunduchi.
 
Sasa Slaa ameingiaje humu??? Acha kuchanganya mada kama una taarifa yako anzisha thread yako kama hyna cha kuchangia ni vyema ukae kimya na usome za wenzako!
 
Mkuu Senior Citizen... Achana na mchumia tumbo huyo, si unajua ni mkwe.re kwa hiyo ana hulka ya kukurupuka na kuropoka, 2015 sio mbali.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom