Makongoro Nyerere amfagilia Profesa Lipumba

Makongoro Nyerere amfagilia Profesa Lipumba

Msulibasi

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2014
Posts
5,957
Reaction score
8,005
Katika Clouds TV nilimuona Makongoro na nikamsikia akisema maneno mazito kwamba Rafiki yangu Ibra---mnamjua Ibra nyie? Professor Lipumba.

Nilikuwa nipo sehemu gani sjui nikamsikia 'anasema wale watu wenye kashfa ya ufisadi badala ya kuwa jela nasikia wamevuta fomu za kugombea kupitia CCM.

Walitakiwa kuwa jela wajifunze kuimba waimbe wengine wapige ngoma zile zinaitwaa waimbe wimbo wa Seya au jeela jeela kubaaya.

Huyu na mpambe wake anataja live .

Nani aliangalia hicho kipindi?
 
Alimtaja Rostam na Lowassa kwa majina kuwa wakaimbe bendi Segerea
 
Makongoro ni mpini kwenye jembe kwasababu anaongea kama mwana wa Afrika, nilimwona na mie hiyo jana na alisema ukweli kama kawaida yake.

Alisema sisi hatuna ugomvi nao ila waache kukipaka matope chama, chama kina watu wenye maadiri wengi ila tatizo ni wenzao wachache ambao wanaharibu taswira ya chama, akasema kamwe watu Wa aina hii hawatakiwi kuwa viongozi kwenye chama wala serikalini.

Nimesoma tena kupitia Mawio alivyokuwa anaongea akiwa Shinyanga, nanukuu .."Waasisi wetu walituambia wanatuachia nchi huru na kutuonya tusije kufanya makosa tukakubali tena kutawaliwa.

Kwani unyonge wetu ulifanya tukatawaliwa, ujinga wetu ndio ulifanya tukanyonywa, lakini leo kwa makusudi tumeamua kurejea kulekule".

Huyu ndo mtu pekee mwenye uchungu na nchi yetu na kama CCM mtaamua kumuleta mwingine kusema kweli mtakuwa mmetusaliti watz.
 
Uzuri wa makongoro hajui kuficha ukweli kama upo lazima usemwe.
 
Anatumia migongo ya watu kupata umaarufu uchwara (cheap popularity) akidhani itamsaidia kwa kuwa ni mtoto wa Nyerere. Haimsaidii akanywe gongo lake shamba
 
Mmenikmbusha akasema pia------Huyu Lowasa anasema hana halipi kisasi---------nani kamfundisha kisasi? anachoo---ametuibia tumemuondoa kwaiyo kisasi ni kuja kutuibia tena-jana ilikua kali sana kutakua na makovu mengi sana baada ya uchaguzi
 
Samaki mmja akioza wote wameoza.Makongoro analalamikia nini ambacho wtz hatufahamu?Wakati hayo majizi yanaiba hela yeye,CCM na serikali yake walikuwa wapi na mpaka sasa hayo majizi kwa kuwa wanayajua wameyafanya nini?Mwaka huu hatudanganyiki hela za CCM tutapokea ila kura hatuwapi.UKAWA ndiyo tumaini letu wa Tanzania.
 
Huyu makongoro sio kosa lake,maji ya makamanda anayo kunywa ndiyo yanampeleka puta.
 
Samaki mmja akioza wote wameoza.Makongoro analalamikia nini ambacho wtz hatufahamu?Wakati hayo majizi yanaiba hela yeye,CCM na serikali yake walikuwa wapi na mpaka sasa hayo majizi kwa kuwa wanayajua wameyafanya nini?Mwaka huu hatudanganyiki hela za CCM tutapokea ila kura hatuwapi.UKAWA ndiyo tumaini letu wa Tanzania.

Umeongea kama layman ...unacomitt fallacy of generalisatio
 
Makongoro ni mpini kwenye jembe kwasababu anaongea kama mwana wa Afrika, nilimwona na mie hiyo jana na alisema ukweli kama kawaida yake.

Alisema sisi hatuna ugomvi nao ila waache kukipaka matope chama, chama kina watu wenye maadiri wengi ila tatizo ni wenzao wachache ambao wanaharibu taswira ya chama, akasema kamwe watu Wa aina hii hawatakiwi kuwa viongozi kwenye chama wala serikalini.

Nimesoma tena kupitia Mawio alivyokuwa anaongea akiwa Shinyanga, nanukuu .."Waasisi wetu walituambia wanatuachia nchi huru na kutuonya tusije kufanya makosa tukakubali tena kutawaliwa.

Kwani unyonge wetu ulifanya tukatawaliwa, ujinga wetu ndio ulifanya tukanyonywa, lakini leo kwa makusudi tumeamua kurejea kulekule".

Huyu ndo mtu pekee mwenye uchungu na nchi yetu na kama CCM mtaamua kumuleta mwingine kusema kweli mtakuwa mmetusaliti watz.

Anaweza kuwa mzee Kigoma maana naye anasema asiyo yatenda , hebu muulizeni Makongoro kwa nini CCM Mkoa wa Mara wanamchukia sana ? Je kweli alivuta kitu kidogo ? Aongelee hilo kabla hatujaweka sawa data .
 
Uzuri wa makongoro hajui kuficha ukweli kama upo lazima usemwe.

Kama baba yake vile ..nakumbuka siku anawashangaa wale wazee waliomwambia akale dili na baba yake ili siku ya uteuzi awepo wampitishe ..Mako akawauliza nyinyi kweli mnamjua Mwl Nyerere? yule mzee ndo ukafanye naye dili? yule hana siri na mtu eti atakuwekea siri ..ndo akasema hilo siwezi, siwezi kula dili na mzee Nyerere tena bora angekuwa mtu mwingine. ...kunaonekana katika familia yao wamekuzwa hivyo, usipende kuwa mwongo na kuwa mwoga wa kubadirisha Maneno, sema ukweli daima.
 
Wamemweka tena hapa star tv wamerudia ile ya clouds makongoro anasema watu wanadaiwa na bodaboda , ni wezi,mafisadi, wasiingie tano bora ,kuna dalili kuwa CCM itapitisha mgombea asiyefaa. hatari sana,kama ni kujiamini nooma , jamaa wakiona hizo clip duuuuuuu, wakichukua nchi? na chama kimesema watu wasishambuliane.anasema dalili ya mvua ni mawingu yaani kuna wingu linatakaa kunyesha lowasa anakaribia ikulu.
 
Anaweza kuwa mzee Kigoma maana naye anasema asiyo yatenda , hebu muulizeni Makongoro kwa nini CCM Mkoa wa Mara wanamchukia sana ? Je kweli alivuta kitu kidogo ? Aongelee hilo kabla hatujaweka sawa data .

Yawezekana na wewe mwenyewe hapo haumpendi, sasa na wewe utatwambia umempa kidogo? mie nadhani tujadiri yaliyopo na kama yapo yanayomhusu basi yalete yajadiliwe kwani unamwogopa nani kuyaleta?
 
MAKONGORO Charles JULIUS KAMBARAGE NYERERE ndiye Amiri Jeshi mkuu Ajaye.
 
DUH JAMAA MMOJA ANA ID 8 MWINGNE 6 MWINGNE 5 owte wanakuja hapa kumzungumzia makongoro... sasa makongoro naye ana akili? nyie mnamwona anavyofanya comedy zake kwa niaba ya membe then mnasema eti anaongea ukweli? mbona mnaikosea sna nchi hiii? makongoro ni vuvuzela tu akipulizwa anatoa mlio hata hajui huo mlio atauchezaje. hana loote ni bora nimchague mwigulu nchemba lakini si makongoro
 
Uzuri wa makongoro hajui kuficha ukweli kama upo lazima usemwe.

nawaonea huruma CCM,kwani wanaosema ukweli hawatakiwi wakati na zama kama hizi nani anataka au atakubali kudanganywa? Makongoro sijapata mfano wake huyu alitakiwa aje huku kwa wenzake-UKAWA
 
Umeongea kama layman ...unacomitt fallacy of generalisatio

Inawezekana wewe ni mwendawazimu hauwajui hawa ma CCM ambao nikama ukoo wa panya,babu mwizi,baba mwizi ,mtoto mwizi hata mjukuu mwizi.Mwaka huu tutawanyoosha hatuichaguui CCM,Chama Cha Majizi.
 
Back
Top Bottom