Uncle Jei Jei
JF-Expert Member
- Jan 7, 2011
- 1,684
- 2,157
Anaandika Makongoro Mahanga
WARAKA MFUPI KWA MKUU WANGU WA MKOA, MH. MAKONDA.
Kuna mambo nimejifunza katika utumishi wangu wa umma na kwenye siasa kwa miaka 40 sasa.
Ni kwamba ukipewa cheo:
1. Kwanza, soma na elewa vizuri mamlaka, madaraka na mipaka yako ya kazi kama yalivyo kwenye instruments za kazi yako na sheria na kanuni zilizopo, na kila siku fanya kazi kwa kuzingatia hayo tu.
2. Pili, pamoja na umuhimu wa kujiamini kwenye utendaji wako, usitumie dharau, majivuno, kiburi na much-know.
3. Tatu, hata kama aliyekuteua au boss wako ni rafiki yako sana, anakusifu na kukupongeza sana, na hata kukupa maagizo yanayokiuka mamlaka yako na sheria zilizopo, lazima ujiongeze ili usitoke kwenye misingi niliyoeleza kwenye namba moja na mbili hapo juu.
Kwa maoni yangu wewe Mkuu wangu wa Mkoa, hujazingatia hizo kanuni za utumishi bora, na ona sasa... wanamichezo na wasanii wanakupinga, wanasiasa na wabunge wa chama tawala na wa upinzani wanakupinga, mawaziri wanakupinga, watumishi wa Mungu wanakupinga, wanasheria wanakupinga, Spika anakupinga, watumishi wa chini yako wanakupinga na sisi wananchi tulio wengi tunakupinga....
....Na kipindi hiki aliyekuwa anakupa ujeuri kutokana na namba tatu hapo juu, atakutosa... na hii ni kwa sababu hukufuata misingi ya namba 1 na 2 hapo juu, na pia hukujiongeza hapo kwenye namba 3 ..... Hakika atakutosaaa kama vile hakujui.. ndivyo walivyo mabosi... chunga maneno yangu haya...
Nduguyo Makongoro Mahanga