Makondakta Dar es Salaam marufuku kusumbua walimu wetu

pierre buyoya

JF-Expert Member
Dec 6, 2015
476
163
Utaratibu wa kutokulipa nauli kwenye vyombo vya usafiri kwa polisi na Wanajeshi umekuwa ni wa kawaida kwa miaka na miaka na umekuwa ukiheshimiwa kweli kweli hasa na wahusika wakutoza nauli hizo (makondata) . . .

Mwaka huu 2016 aliyekuwa mkuu wa wilaya ya kinondoni sasa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda alijitahid kuongea na wadau na kufanikisha mchakato wa kuwafanya walimu wa mkoa wa Dar es Salaam kupanda bure daladala jijini hapo . . .

Shida imekuja hapa, Makondakta wa dadadala wamekuwa wakitoa kauli ambazo zinawafanya walimu kujiona kama wako tofauti ndani ya vyombo hivyo vya usafiri. Kauli ambazo zinalenga kuwafanya waalimu waone haya kutembea kifua mbele kama wao ndio waalimu wanaopaswa kupanda bure daladala . . .

Sasa nyie makondakta tunaomba muwaache waalimu wetu wawe na uhuru wakutumia fursa hyo ambayo maboss zenu wamewapa, muwaheshimu kama mnavyoheshimu polisi na wanajeshi wakiwa kwenye daladala . . .

Makondakta hamna mamlaka ya kusumbua waalimu.

6f8554115cc85fdccaf26c4f916497b4.jpg
 
kondakta:haya muda wa kugawana ridhki umefika andaeni nauli!
mwalimu:mimi mwalimu

kondakta:eek:nyesha kitambulisho!

mwalimu:(anatoa kitambulisho) hiki hapa

kondakta:mbona umekaa?

mwalimu:kwahyo nisimame?

konda:ndo mana ake dogo mwanafunzi huyu ametoa 200 na kasimama sembuse wewe unakalia siti bure (mwalimu anaamua kutoa tu hyo 400
 
Hii inaniuzi serikari kukwepa majukum yake.serikari iwaongezee mishahara kwa 50% walipe nauli.ukiingiza gali ya biashara ushulu wake ni mkubwa ulipe bima,mapato,sumatra,police,veta,halafu wanasema eti usafilishe walim, police,wanajeshi bure huo ni upuuzi.
 
shida za walimu tz kote sio nauli za daladala shida za walimu ni mishahara duni pamoja nakufanya kazi kwenye mazingira magumu,,,msiwatumie walimu kujinufaisha kisiasa jamani.
 
Mleta uzi wewe hangaika na buku 7 yako na siasa zenu.mimi nafanya biashara ya daladala nimewambia madereva na makondakta wangu ni marufuku kupakia mwalimu bure.nimenunua gari zangu milioni 60 kila moja spare mipira matrafiki wanasumbua vibari na matakataka mengine hakuna siku serikali imenionea huruma.nimewaambia ni marufuku mwalimu kupanda bule na atakae mkamata hiyo kesi itakuwa mfano kwa walimu wote.huyo Mabrouk anakubari walimu wapande bule ana daladala moja tu mwenyekiti gani hajielewi au wasubiri shangingi la makonda wapande
 
Daladala zako znapga rout ya wapi Mkuu? Nataka nikapande then unishushe ili niamini kama kweli we ni mtata,nicjekuwa unawakazia walimu wa like then unaleta tambo hapa
 
Tandika segerea Tandika muhimbili kinyerezi Rozana Segerea ubungo nimewambia ni marufuku kupakia mwalimu atakaemkamata kwa kumkataa mwalimu aniambie atanilipa hesabu za mwaka mzima.Polisi Jwtz magereza walemavu wote wanapanda bule na walimu nao wapande bule aaa kwangu hapana hii ni biashara kwa nini na madukani wasipewe vyakula bule huyo Mabrouk ana gari moja tu ndio maana anaona haumii
 
kondakta:haya muda wa kugawana ridhki umefika andaeni nauli!
mwalimu:mimi mwalimu

kondakta:eek:nyesha kitambulisho!

mwalimu:(anatoa kitambulisho) hiki hapa

kondakta:mbona umekaa?

mwalimu:kwahyo nisimame?

konda:ndo mana ake dogo mwanafunzi huyu ametoa 200 na kasimama sembuse wewe unakalia siti bure (mwalimu anaamua kutoa tu hyo 400
Makonda wapumbav sana, Huu utaratibu wa kawaida kwa wanajeshi na polisi ila kwa walimu wanasumbuliwa.
 
Hii inaniuzi serikari kukwepa majukum yake.serikari iwaongezee mishahara kwa 50% walipe nauli.ukiingiza gali ya biashara ushulu wake ni mkubwa ulipe bima,mapato,sumatra,police,veta,halafu wanasema eti usafilishe walim, police,wanajeshi bure huo ni upuuzi.
Ila wadau wa usafirishaji wamekubaliana na mkuu wa mkoa ina maana wameona faida bado itakuwepo, sion swala la kucomplain ni kutimiza wajibu tu.
 
Mleta uzi wewe hangaika na buku 7 yako na siasa zenu.mimi nafanya biashara ya daladala nimewambia madereva na makondakta wangu ni marufuku kupakia mwalimu bure.nimenunua gari zangu milioni 60 kila moja spare mipira matrafiki wanasumbua vibari na matakataka mengine hakuna siku serikali imenionea huruma.nimewaambia ni marufuku mwalimu kupanda bule na atakae mkamata hiyo kesi itakuwa mfano kwa walimu wote.huyo Mabrouk anakubari walimu wapande bule ana daladala moja tu mwenyekiti gani hajielewi au wasubiri shangingi la makonda wapande
Vp mkuu hujawapiga marufuku kuwapandisha Wanajeshi na polisi bure???
 
Back
Top Bottom