Emc2
JF-Expert Member
- Sep 26, 2011
- 16,808
- 16,881
[HASHTAG]#TEAMMAKONDA[/HASHTAG]
Huu usemi wa mkuu wa mkoa wetu wa Dar es salaam umeanza kuonesha matunda yake. Naona kila rangi na aina ya nyoka watoka baada ya jana. Tayari wengi wameanza kutoa matamko mbalimbali baada ya kuitwa kituoa cha polisi.
Nachelea kusema kwamba huenda ndugu zetu hawa wanaopiga kelele baada ya jana wanajua siri kubwa.
Sasa hivi tunaona picha ya kila nyoka akitokeza kwenye shimo. Huko bungeni nako kunanyoka wameanza kutoa vichwa vyao. Kila mmoja natoka akiwa amejificha kwa kutumia mgogo wa sehemu alipo. Jana bungeni moto umewaka huku wengine wakitoa mifano ya Jairo na kadharika. Wanaongea mishipa imewakakamaa.
Kipindi hiki naomba serikali ikaze hawa wanaizoea serikali na kuishika sharubu. Iweje uitwe kituo cha police uanze kung'aka. Si uende ujue unaitiwa nini. Kama tuhuma hizo zinakuhusu kesi itaenda mahakamani na utasikilizwa. Ukituhumiwa nenda ukahojiwe kwa ajili ya usalama wa nchi yetu.
Kumbuka vijana wengi sana wemeharibika kwa madawa haya. Night Clubs zimekuwa zinatumika sana. Iweje wamiliki wa night clubs zingine waende kimya kimya lakini mmiliki wa Bills atetewe na chama?