Makonda: Tabia yangu inajulikana, sina tabia ya kukuchekea wakati moyoni nimekununia

Makonda: Tabia yangu inajulikana, sina tabia ya kukuchekea wakati moyoni nimekununia

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
2,434
Reaction score
5,228
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Paul Makonda ametaka watendaji wa Wizara hiyo kufunga mkanda ili kutimiza malengo waliyojiwekea wakiwa chini ya Profesa Palamamba Kabudi.

Makonda ameyasema hayo hii leo tarehe 13 January 2026, kwenye zoezi la kukabidhiwa ofisi muda mchache mara baada ya kuapishwa na Rais Samia Suluhu Hassan Ikulu Chamwino, Dodoma.

Makonda amesema kuwa watendaji wa Wizara hiyo wanatakiwa kufunga mkanda kwa kuwa tabia yake inafahamika na ndio iliyomfikisha hapo.

"Naomba watendaji wa Wizara kila mtu akae kwenye siti yake kwa kuenea na afunge mkanda kwa kuwa tabia yangu inajulikana, sina tabia ya kukuchekea wakati moyoni nimekununia," amesema Makonda.
 
Back
Top Bottom