Makonda na mikakati yake iliyomsaidia kuwajibika katika matokeo mabaya sana ya kidato cha nne

Tizzo G

Member
Jun 9, 2012
25
17
Kwa habari za kawaida na mtazamo wa kweli ni kwamba ndg Paul Christian Makonda aliekua anaitwa Daudi Albert Bashite miaka ya 2000 kurudi nyuma alitumia mwanya wa kutangaza majina ya watu wanaotumia na wanaojihusisha na uuzwaji wa madawa ya kulevya kwa sababu zifutazo;-
(i) kwanza aliyataja majina yale ya wahusika wa madawa ya kulevya kwa lengo la kuhadaa umma ili usahau matokeo ya kidato cha nne na kutokuyajadili.
(ii) pili kuufanya usihoji uwepo wa shule sita za Dar-es-salaam katika shule kumi zilizoshika mkia katika matokeo ya kidato cha nne.
(iii) tatu kuepuka kuwajibishwa na kuwawajibisha wausika kama walivyowajibishwa wahusika katika mkoa wa mtwara kwenye matokeo ya darasa la saba pale shule za mtwara zilipokua za mwisho, kwani watu walikua wanatazamia yatafanyika kama yaliyofanyika kule mtwara.

(iv)nne, kufunika madudu yaliyofanywa na shule za serikali, ikumbukwe katika shule 50 bora hamna ya serikali hata moja, je watoto hawa wa watanzania maskini wataishia kufeli tuu? maana wengi wao ndio wanaosoma shule za serikali na hasa za kata.
ila bunge letu halikuweza kuhoji hilo kwani walibaki na kukumbatia madawa ya kulevya wakasahau kuangalia masuala ya elimu ambayo yangeweza kutupatia wataalamu wa kushughulika na madawa ya kulevya na weledi mkubwa sio kama wa huyu RC makonda a.k.a Bashite.

Watanzania wenzangu tuwe makini na headlines za kila siku, tuangalie malengo ya kitaifa kwanza, elimu bora ndio suluhisho la kila tatizo maana watu watafikiri madhara ya jambo kabla ya kutenda.
Tufikirie Taifa letu linaenda wapi kielimu kwanza ili tuepuke kuwa na watu akina Bashite ambao wanaweza kuhatarisha amani ya nchi yetu kwa kukosa maadili ya utendaji kazi yasiyojali umri, hadhi ya mtu pamoja na utu wa mtu. Together we can.
 
Kuna madudu mengi kwenye maadili ya viongozi wateule, japo utaona kimya, hakuna kuchukua hatua. Naifananisha hali hii na ile iliopo kambare republic, baba mama mtoto wote wana ndevu.
 
Back
Top Bottom