Makonda kuwa Mgeni Rasmi siku ya Wanawake Duniani

Brigedia Chan-ocha

JF-Expert Member
Mar 7, 2014
1,353
2,842
Tarehe 8 march mwaka huu, mkuu wetu wa mkoa wa Dar anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yatakayofanyika kwenye uwanja wa Mwembeyanga TEMEKE jijini Dar.

Hii ni kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar. Katika taarifa hiyo, maadhimisho hayo yataongozwa na maandamano ya wanawake na wadau mbalimbali na yataanzia shule ya msingi Mabatini kuelekea viwanja vya Mwembeyanga.

==================
Habari Zaidi

Taarifa hii imetolewa na Idara ya habari maelezo Dar es salaam Tanzania ambayo iko chini ya Wizara ya habari, sanaa, utamaduni na michezo na imeandaliwa na Mwandishi wa Idara hiyo Immaculate Makilika.

Taarifa ni kwamba Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani yanayotarajiwa kufanyika Machi 8 Mwaka huu katika uwanja wa Mwembeyanga Temeke Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa iliyoandikwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, maadhimisho hayo yataongozwa na maandamano ya Wanawake na wadau mbalimbali na yataanzia katika Shule ya msingi Mabatini kuelekea viwanja vya Mwembeyanga.

Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani mwaka huu yanaongozwa na kauli mbiu isemayo “Tanzania ya viwanda, Wanawake ndio msingi wa mabadiliko ya kiuchumi ikilenga kuikumbusha jamii kuhusu umuhimu wa kujenga mazingira wezeshi kwa Wanawake hasa kutambua mchango wao katika kuleta Maendeleo yao na ya jamii kwa ujumla.

Maadhimisho hayo yataambatana na maonesho ya kazi za ujasiriamali yanayoendelea katika uwanja wa Mwembeyanga, ambapo Asasi za kiraia na vikundi mbalimbali vya Wanawake vitaonesha bidhaa zao.

Screen-Shot-2017-03-07-at-5.09.31-AM.png
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani yanayotarajiwa kufanyika Machi 8 Mwaka huu, katika uwanja wa Mwembeyanga Temeke Jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam jana maadhimisho hayo yataongozwa na maandamano ya Wanawake na wadau mbalimbali, na yataanzia katika Shule ya Msingi Mabatini kuelekea viwanja vya Mwembeyanga.

Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Mwaka huu yanaongozwa na kauli mbiu isemayo “Tanzania ya viwanda, Wanawake ndio Msingi wa Mabadiliko ya Kiuchumi”.

Kauli mbiu hiyo inalenga kuikumbusha jamii kuhusu umuhimu wa kujenga mazingira wezeshi kwa Wanawake hasa kutambua mchango wao katika kuleta Maendeleo yao na ya jamii kwa ujumla.

Taarifa hiyo pia imeikumbusha jamii kuhusu wajibu wake ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha, kuwaamini na kuwapa Wanawake haki sawa katika nafasi za Elimu, Uchumi na uongozi ili wawe chachu ya mabadiliko yenye lengo la kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda.

Maadhimisho hayo yataambatana na maonesho ya kazi za ujasiriamali yanayoendelea katika uwanja wa Mwembeyanga, ambapo Asasi za kiraia na vikundi mbalimbali vya wanawake vitaonesha bidhaa zao.

Aidha, Wananchi wa Mkoa wa Dar es salaam wanakumbushwa kushiriki kwa wingi katika maadhimisho hayo ikiwa ni pamoja na kuwa na mikakati ya kukabiliana na changamoto mbalimbali zinanazowakabili Wanawake kuanzia ngazi ya kaya hadi Taifa.

Mwisho.

Kesho tarehe 8 ambayo ndio kilele cha maazimisho ya siku ya wanawake dunia, kimkoa Dar es salaam sherehe hizi zitafanyika Temeke viwanja vya mwembe yanga!

Wana Dar es salaam tujitokeze kwa wingi siku hii muhimu kwa wanawake na jamii kwa ujumla.

My take, Makonda yupo hapa hapa mjini na hao waliomuona south watakuwa na Makonda wao!
 
Tata Makonda katika ubora wake
 
Amealikwa kwa Madiba kuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za siku ya wanawake duniani.Kwa bongo atawakilishwa na Kaimu.
Sadiki Ukipenda.
Ova.
 
Taarifa hii imetolewa na Idara ya habari maelezo Dar es salaam Tanzania ambayo iko chini ya Wizara ya habari, sanaa, utamaduni na michezo na imeandaliwa na Mwandishi wa Idara hiyo Immaculate Makilika.

Taarifa ni kwamba Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani yanayotarajiwa kufanyika Machi 8 Mwaka huu katika uwanja wa Mwembeyanga Temeke Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa iliyoandikwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, maadhimisho hayo yataongozwa na maandamano ya Wanawake na wadau mbalimbali na yataanzia katika Shule ya msingi Mabatini kuelekea viwanja vya Mwembeyanga.

Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani mwaka huu yanaongozwa na kauli mbiu isemayo “Tanzania ya viwanda, Wanawake ndio msingi wa mabadiliko ya kiuchumi ikilenga kuikumbusha jamii kuhusu umuhimu wa kujenga mazingira wezeshi kwa Wanawake hasa kutambua mchango wao katika kuleta Maendeleo yao na ya jamii kwa ujumla.

Maadhimisho hayo yataambatana na maonesho ya kazi za ujasiriamali yanayoendelea katika uwanja wa Mwembeyanga, ambapo Asasi za kiraia na vikundi mbalimbali vya Wanawake vitaonesha bidhaa zao.

Screen-Shot-2017-03-07-at-5.09.31-AM.png

Chanzo: Alipoalikwa kesho Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda - millardayo.com
 
Kwani kuna Mkuu wa Mkoa wa Dar mwingine?

Na tunajua ikitokea kiongozi yaani mfano wakuu wa Mikoa yupo safari au likizo, basi mtu mwingine ana kaimu kama kawaida.
 
Kuna watu naona hamuamini kama taarifa hii ni ya kweli, jamaa yupo!
 
Back
Top Bottom