Makonda: Baadhi ya ombaomba wanauza ‘unga’

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
MKUU wa Mkoa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kwa mujibu wa utafiti alioufanya, ombaomba walioko jijini Dar es Salaam baadhi yao wanajihusisha na uuzaji wa dawa za kulevya. Akihojiwa katika mahojiano ya moja kwa moja na kituo kimoja cha redio, Makonda alisema wapo watu ambao wanatumia mwanya huo kusambaza dawa za kulevya.

“Wapo wanaotumia fursa hii kusambaza dawa za kulevya kwa sababu anavyopita huwezi kumhisi kwa namna anavyoonekana, lakini watu hawa ni miongoni mwa mawakala wa kusambaza dawa za kulevya,” alisema Makonda.

Makonda aliwataka wakazi wa jiji hilo kushirikiana naye katika kuwaondoa ombaomba hao ambao wengi wanatoka nje ya Da es Salaam na kwamba hakuna tija kuendelea kuwaacha. “Watanzania tuna upendo sana lakini tunahitaji kutafakari kama kweli watu walioko barabarani wakiomba kama kweli wanahitaji msaada huo au la,” alisema Makonda.

Alisema kwa kuendelea kuwaacha ombaomba hao pia kutasababisha vijana ambao sasa wanaomba barabarani kuwa watu hatari katika maisha yao ya baadaye kwani wakikosa pesa wataingia katika shughuli za uporaji ili wapate fedha.

“Itafika kipindi ataanza kuangalia kile alichokuwa anakikusanya wakati akiomba na kile anachokipata akifanya kazi, ataona akifanya kazi hapati kiasi kikubwa, ataamua kuwa mporaji,” alisema Makonda.

Makonda alisema kwa mujibu wa utafiti alioufanya, asilimia 80 ya ombaomba wanatoka nje ya Dar es Salaam na kesho operesheni ya kuwaondoa watu hao itaanza rasmi huku wale ambao hawana ulemavu wowote wakikamatwa kwa makosa ya uzururaji.
 
Makonda kwa omba omba sawa wewe Pambana nao tu hadi mwisho hope utashinda! Ila suala la parking kwa wenye magorofa na sensa ya watu wote wa Dar hizo ndoto! Labda uwe na fungu kabisa lakini usiwapelekeshe watendaji wa mitaa ambao hata hawalipwi wafanye hilo zoezi gumu na lisilo na tija sana kwa mantiki ya kuwatafutia kazi au ca kufanya! Kupata wasio na kazi sio lazima uitishe senda ya nyumba kwa nyumba! Waite tu watakuja au weka vituo vya kuwasajili kwenye wilaya zako uone! Hivi una bajeti ya kusaidia nyumba Mil 1 na wakazi wake? Mfano kila nyumba iwe na mtu 1 anaehitaji msaada wako kupata hizo kazi unazodai utawapa! Watu Mil 1.....unakumbuka ndio ilani ya JK kwa miaka 5 nchi nzima? Punguza papara na porojo!
 
Makonda yukosawa kabisa NA sio TU madawa hii n Ukweli ulizeni wale watoto wa kiume Wa pale mnazimmoja wengi huchukuliwa NA wafanyabiashara NA kwenda kufanywa kinyume NA maumbile nakupewa pesakubwa TU

NA wengine huchukuliwa NA waarabu NA kwenda kuwafanya nw kulipwa hela kubwa TU sana TU.......KUNA NGO waliwahi kwenda kuwahoji wakadai wakatiwegine wanachukuliwa wakawafanye hao wafanyabiashara.....kuwaacha n. Kuwaambukiza magonjwa
 
Acheni porojo, wauza ngada na ndumu ni wale wanaojifanya vichaa, huku kwetu eneo la mkuyuni kwa mswahili yupo mwehu pale ana mbwa kama ishirini kazi yake ni kuuza misokoto ya ndumu, vijana wote wa shede huwa wanaenda kupiga puli pale, hawa wazee waliokimbia maisha magumu nungwi ni kuwaonea tu.
 
Back
Top Bottom