Egnecious
JF-Expert Member
- Jul 8, 2015
- 875
- 960
MAKONDA AMFAGILIA DC HAPI KIAINA KWA JPM
*Asema alipokaimu ameonesha cheche kali
*Amwambia JPM likipatikana jukumu kubwa zaidi anatosha
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh. Paul Makonda amempigia debe Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Hapi mbele ya Rais John Pombe Joseph Magufuli leo.
Akitoa salamu za Mkoa wa Dar es Salaam kwa Rais Magufuli, wakati wa kuwatambulisha wakuu wa wilaya za Dar es salaam, Makonda alimwambia Mh. Rais kuwa ana imani kubwa nao na kwamba kwa upekee katika kipindi cha mwezi mmoja wa kukaimu DC Hapi ameonesha uwezo mkubwa.
"Mh. Rais umejionea mwenyewe wakati nilipokua likizo, Kaimu RC alivyokuwa anatema cheche. Ni ukweli usiopingika kuwa anao uwezo mkubwa na ikitokea nafasi kubwa zaidi basi Mh. Rais uelewe kuwa una hazina hapa..." Alisema Makonda.
Rais Magufuli leo amezindua mradi wa mabasi ya mwendokasi - DART eneo la Kariakoo gerezani.