Makomando wa Mmarekani wavamia Ngome ya Al-Qaeda nchini Yemen

Good People

JF-Expert Member
Aug 6, 2016
945
1,819
Ripoti kutoka Yemen, zinaeleza kuwa shambulio,
lililofanywa na makamando wa Marekani,
limeuwa watu kama 30, wanaoshukiwa kuwa
wapiganaji wa al-Qaeda na raia.
Hata hivyo jeshi la Marekani linasema kuwa
kamando wake mmoja, aliuwawa, na wengine
watatu walijeruhiwa, katika shambulio dhidi ya
makao makuu ya al-Qaeda nchini Yemen.
Ndege ya jeshi la Marekani iliyotumika katika
shambulio hilo, ilielezewa kuwa ilitua kwa
kishindo, na kujeruhi wanajeshi zaidi.
Jeshi linasema wapiganaji 14 waliuwawa, katika
shambulio hilo lilofanywa alfajiri, katika jimbo la
al-Baida.
Lakini watu wa huko, wanasema idadi ya
waliouwawa ilikuwa kubwa zaidi, na wanasema
raia kadha pia waliuwawa.
Wadadisi wanasema, shambulio hilo la kwanza la
aina yake, tangu Rais Donald Trump kuapishwa,
litaonekana kama ishara ya lengo lake la
kutumia nguvu zaidi dhidi ya makundi ya
wapiganaji wa Kiislamu.
 
Ni awamu nyingine tena tutashudia mnyukano na mtifuano mkali kati ya mbabe USA na WAFIA DINI AKA MAGAIDI.
Ila tafadhali mstituingize sie WAMATUMBI kwenye bifu zenu.
 
Kama kawaida ya marekani ;

Democrats wanakusanya pesa,

Republicans wanazitawanya kwa vita.
 
Nadhani kuna kitu hakiko wazi hapa.. Marekani ni sehemu tu ya timu ya mataifa nguli ya kiislam yanayopingana huko Yemen. Wa Saudi Arabia (wa sunni) hawataki wairan( wa shia) watawale Yemen. Kwahiyo Saudi Arabia imepeleka majeshi na kutembeza kichapo huko Yemen dhidi ya waasi wanaoungwa mkono na Iran
 
Back
Top Bottom