hamis77
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 18,679
- 27,656
Msikiti wa Majini (Masjid al-Jinn) ni moja ya sehemu za kipekee mjini Makkah.
Mzee wangu alienda mwaka Jana kufanya hijja , nilimuuliza akasema huo MSIKITI ni kweli una matukio na VITUKO vya majini , kila siku Namuombea Mzee wangu kabla hajalala mauti atoke huko .
Nimeona Leo niwajuze kuhusu huu MSIKITI ambao unaitwa Masjid Al jinn, Ingawa si miongoni mwa misikiti mikubwa, ila unatambulika sana kwa sababu ya tukio la kihistoria lililotokea hapo, ambapo Muhammad alikutana na kundi la majini waliomsikiliza akisoma Qur’ani, kisha wakaamini akawasilimisha.
Tukio hili limeelezwa ndani ya Qur’ani, katika Sura ya Al-Jinn (72).
Qur’ani inasema wazi kuhusu majini walimsikiliza Muhammad wakaikubali Quran na kundi hilo la majini likasilimu.
(Qur’ani 46:29).
Hadith pia zinasimulia kuwa Mtume alisoma Qur’ani na majini wakakubali Uislamu.
Tukio hili ndilo lililoufanya msikiti huu kuwa maarufu sana,
Msikiti huu ulijulikana tangu karne ya 7 kutokana na tukio hilo la muhamad kuyasilimisha majini, lakini ujenzi wake rasmi ulifanywa karne nyingi baadaye chini ya utawala wa Waislamu wa Hijaz.
Baadaye Serikali ya Saudi Arabia iliuendeleza ili kuhifadhi kumbukumbu hii ya kihistoria.
📌 Kwa nini Unaitwa Msikiti wa Majini?
Unaitwa hivyo kwa sababu ya tukio la kihistoria ambapo majini walimsikiliza Muhammad akihutubu na kusoma Qur’ani usiku.
Baada ya kuisikia, waliamini na wakaahidi kuwaonya majini wenzao.
Tukio hili liliweka wazi kwamba Qur’ani si kwa waislamu pekee bali pia ni ujumbe kwa majini yaliyofukuzwa mbinguni .
📌 Visa vya Watu Wanaoingia Msikitini
Kuna simulizi nyingi kutoka kwa mahujaji na wageni
Wengi wanasema walisikia sauti za Qur’ani bila kuona mtu.
Wengine walihisi kama wako katikati ya kundi kubwa la watu, kumbe msikiti uko mtupu.
Wengine waliona mwanga wa ajabu usiku, kana kwamba ibada inaendelea.
📌 Visa vya Sheikh Hashim Rusaganya
Sheikh Hashim Rusaganya, miongoni mwa masheikh maarufu Tanzania, aliwahi kusimulia visa kadhaa kuhusu Msikiti wa Majini:
Kisa cha Kijana Hujaji
Kuna kijana aliyekwenda kuswali Msikiti wa Majini usiku baada ya kutoka Haram. Alipoingia, alihisi kama msikiti umejaa watu wakiswali pamoja naye. Alisikia sauti nzuri za Qur’ani zikisomwa kwa Sauti ya madaha, Lakini baada ya kuswali na kugeuka nyuma, aliona kuwa yuko peke yake msikitini.
Kisa cha Mahujaji Wawili
Mahujaji wawili vijana kutoka Afrika waliingia msikitini usiku. Walihisi kama msikiti umejaa, na waliposwali, waliposoma Qur’ani wakasikia yakijibu “Amin.” Walipomaliza swala na kugeuka nyuma, waligundua kuwa walikuwa peke yao.
Kisa cha Mwanamke Hujaji
Mwanamke mmoja alipotea njiani usiku karibu na msikiti. Alionekana kuongozwa na mwanamke mwenzake hadi karibu na mlango wa msikiti. Alipogeuka kumshukuru hakuwepo tena.
Sheikh Rusaganya alifundisha kwamba alikuwa ni jini kwa ruhusa ya Allah.
Kisa cha Sauti ya Qur’ani
Mtu mmoja aliyelala karibu na msikiti alisikiliza Qur’ani ikisomwa kwa sauti kubwa kana kwamba msikiti umejaa. Lakini alipoamka na kuangalia, aliona kimya kabisa. Sheikh alisema, “Haya ndiyo mambo yanayothibitisha kuwa Msikiti huu bado unatumiwa na majini hadi leo.”
📌 Visa Vingine vya Masheikh wa Tanzania
1. Sheikh Yahya Hussein (Dar es Salaam)
Aliwahi kueleza kuwa Msikiti wa Majini ni ushuhuda wa kwamba ibada haikuwekewa mipaka kwa binadamu pekee. Aliwahi kutaja simulizi za mahujaji waliopata “msaidizi wa ghafla” karibu na msikiti – mtu asiyejulikana aliwaongoza njia au kuwasomea du‘a, kisha akatoweka.
2. Sheikh Othman Maalim (Tanga)
Alisimulia kuwa mahujaji kutoka Tanzania walimwambia walipoingia kuswali Msikiti wa Majini, walihisi kama wameswali kwa “umati mkubwa” hata kama walikuwa wachache.
3. Sheikh Salum Barahiyan (Zanzibar)
Katika mawaidha yake kuhusu masuala ya majini, alitaja Msikiti wa Majini kama alama ya ushahidi wa Qur’ani kuwa majini wapo. Alisema simulizi za watu kusikia sauti za Qur’ani ndani ya msikiti huo si jambo la ajabu, kwa kuwa Qur’ani inasema wazi kuwa majini waliisikia na kuamini.
Swali linakuja ,Kwanini Majini yaliposikia Quran yakaikubali na yakasilimu na kuwa waislamu?
Nimewahi kukutana na Binti mmoja ambaye ni dada wa kazi wa jirani yangu, siku moja wakampeleka kanisani kama mgeni tu ,siunajua wengi Huwa wanawapeleka kanisani wadada wa Kazi,
Mziki ulianza aliporudi ,bint akapagawa na hilo Jini ,lilikuwa linadai halitaki kabisa lipelekwe huko kanisani Tena ,Bali linataka kwenda msikitini tu, yule bint alikuwa anaitwa mariamu, katika kulihoji Jini lililo ndani yake likawa linasema linaitwa Rahma ,
Nikashauri TUFANYE maombi ,bahati mbaya yule dada ambaye ndiye bosi wake ,akaharakisha kumrudisha yule Binti kwao mkoani ,
SWALI NINALOJIULIZA MPAKA KESHO KWANINI MAJINI YALIONA QURAN NA UISLAMU NDIO SAHIHI KWAO ?
Bado nasoma kujua rank za mapepo ,majini kwa UPANDE Wa shetani ,
Yesu aliwahi kuwaambia wanafunzi wake waliposhindwa kumtoa Pepo ,alisema kwa aina hii halitoki labda ufunge au maombi , it means kwamba Kuna Pepo au Jini unalifukuza kwa kukemea tu, ila Kuna aina (kinds) inahitaji njia zaidi, ...ukisoma Mathayo 17:21
Matthew 17:21 KJV
[21] Howbeit this kind goeth not out but by prayer and fasting.