Makinda, Ni kweli bunge halina nafasi ya kuishauri Serikali?

Criterion

JF-Expert Member
Jan 8, 2008
11,796
11,882
Wanajamvi,

Kwa mara nyingine tumeshuhudia utata usiokuwa wa lazima, unaotengenezwa makusudi kwa gharama ya kodi za watanzania, ili kuhujumu raslimali za taifa.

Kilichonisikitisha jana si hatima ha kikao hicho cha bunge, bali ni yale yaliyokuwa yakijiri ndani ya chombo hicho ambayo, pamoja na kusitishwa kwa bunge na kuongeza matumizi ya bunge yasiyo ya lazima, pia ni msingi mkubwa wa kuhitimisha umoja wa kindugu, uhusiano mwema wa watawala na raia, misingi na maadili ya watumishi wa uma, uwajibikaji wa viongozi na tegemeo la wananchi kwa serikali ndani ya Tanzania. Sintofafanua haya kwa sasa lakini ninaamini wanaopenda kuelewa, wameelewa.

Pamoja na hayo, pengine ndiyo hatima ya tanzania na serikali ya ccm, kama alivyosema kakobe, ndiyo hitma yake inakuja kwa dizaini hii. Lakini ninaomba ufafanuzi wa mambo yafuatayo. Ninaomba tujadili bila jazba, wala ushabiki wowote wa vyama vya siasa, ama maslahi ya utawala:-

1. Ni kweli kwamba benge haliruhusiwi kuishauri serikali nini cha kufanya? Kama ndivyo, nini maana ya kuwa na bunge linalotumia fedha za walilpa kodi ikiwa halina uwezo wa kufanya maamuzi yakuisaidia serikali kufanya vizuri?

2. Maadam spkeaer, ni nini kililipa bunge nguvu kuipa serikali ushauri na hatua za kuchukua dhidi ya similar if not weaker cases zilizotangulia hili ambazo serikali ilizifanyia kazi bila uadui huo huwepo? Ni kweli bunge hlaina uwezo huo au moyo wako na mafisadi ndiyo hauna uwezo na utashi huo?


3.. Makinda amekuwa akisema ana migogoro na mahkama, hivo hahitaji kuwa na migogoro na serikali. Mahakama gani anamigogoro nayo? Mahakama ni nini? Mama speaker anathamini uhusiano wake na hao majudge watatu waliofanya kazi in favor of mafisadi wachache, kuliko wajibu wake na kiapo chake cha kusimamia maslahi ya taifa lenye watu takribani 50m sasa? Uzalendo wa mama skpika uko wapi?

4.. Mama spkear anaogopa kuwa na mgogoro na serikali ikiwa atasimamia haki za nchi. Haoni kwamba anaonyesha ni namna gani yeye ni kibaraka wa watawala? Kwamba kwa kukubali, bunge liishauri serikali iwafute kazi, kuwashitaki na kuwafilisi mafisadi na wazembe, atakuwa adui wa serikali. Hapa si dhahiri kwamba ufisadi, wizi na uzembe KUMBE ndiyo sera ya serikali?

5. Pamoja na hayo, sasa wazalendo wa nchi hii bila kuajli vyama wala dnini wala age waka kabila, tuunganishe na tuhuma za kikwete na familia yake juu ya ufisadi, na ushahidi uliotolewa kwama kikwete ndiye aliamrisha fedha zitoke, na vile watuhumiwa vile walivyofurahi walipozungumziwa nini cha kuwafanya aachiwe kikwete.

Baada ya hapo, tuone namna PAC walivyosema kwamba wanamwacha raisi kwa sababu wakimgusa nchi itayumba. Na bila kumung'unya, raisi kikwete ni mafia anayeongoza kundi la mafisadi kwa ndani, akitoka nje anawalaghai watanzania, halafu anarudi ndani kwenda kulinda kundi lake na kimafia na kifisadi.

Kwa mtazamo huu, ninaomba tuzungumze bila aibu,

1. Je ni kweli kikwete anasimamia na kuitetea, na kuilinda katiba ya nchi sawa na kiapo chake?

2. Ni kweli Pinda hana hatia katika scandle ya escrow?

3. Wakuu wa idara na viongozi mbali mbali watakao kuwa butu katika kazi zao, wakapotoshwa na wachini yao, nao waschukue hatua yoyote ya kujipa ufahamu na kuwawajibisha wa chini yao, kuanzia sasa hawatachuliwa hatua? Kiongozi anaposhindwa kusimamia ofis yake ikafanya vizuri, ni kweli kwmba hana hatia? Ni nini maana ya uwepo wa viongozi? pinda kama waziri mkuu, madudu yote yanafanyika mbele yake, yeye amekazana kuua na kupiga wapinzani hku kumbe kazi zake haziendi ipasavyo, bado anasifa ya kuendelea kukalia ofisi?

4 USHAURI WANGU NI KWAMBA, HATUA ZA KUTOKUWA NA IMANI YA KIKWETE, WAZIRI MKUU ZICHUKULIWE ILI WAIACHE NCHI ITIBU MAJERAHA WALIYOYASABISHA. WATAKAPOACHWA WAENDLEE KUWEPO MADARAKANI, KUFIKIA MWAKA KESHO, WATAKUWA WAMESHAIMALIZA HII NCHI WAKIJUA FAMILIA ZAO NA MAFISADI WENZAO WAKO SALAMA.

NCHI INATIKISIKA TANGIAPO NA HAKUNA MTIKISIKO ZAIDI YA ULIOPO NA PENGINE WATAFANYA MTIKISIKO MKUBWA KULIKO TULIOKWISHA UONA. NI AFADHALI KUORGANIZE A THOROUGH HANDLING OVER HAWA WATU WAOENDOKE, KULIKO MAZINGIRA YA VURUGU WANAYOYATAYARISHA.
 
Back
Top Bottom