Makinda ahimiza ukakamavu kwa wanawake

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,570
9,432

pic+makinda.jpg



Spika mstafu, Anna Makinda amesema kuna haja ya kuwajenga kikakamavu wasichana katika umri mdogo ikiwa ni njia ya kuwaanda kuwa viongozi wa baadaye jambo ambalo litasaidia kufikia 50/50 katika nafasi za uongozi wa nchi.

Makinda amesema hayo leo Jumatano wakati wa Kongamano la Kigoda cha Mwalimu Nyerere linaloendelea katika Ukumbi wa Nkuruma, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Maudhui ya kongamano hilo kwa mwaka huu ni nafasi ya wanasiasa katika kuanguka na kuinuka kwa maendeleo ya bara la Afrika lakini mada ndogo ya leo ni mwanasiasa mwanamke na harakati za usawa wa kijinsia.

"Kuna haja ya kuwafundisha ukakamavu wanawake tangu wakiwa wadogo kwa sababu katika vyama vya siasa wanawake wapo wengi lakini kazi yao kubwa ni kuimba nyimbo za vyama na kupika chakula wakati wa mikutano badala ya kufikiria na wao kuwa viongozi," amesema Makinda wakati akichangia mada.


Chanzo; Mwananchi
 
Back
Top Bottom