Makinda against sitta! Kazi kweli!

Makinda against sitta! Kazi kweli!

Joined
Sep 21, 2012
Posts
25
Reaction score
4
SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda na Naibu Spika, Job Ndugai, wanasemekana kutumiwa na maadui wa demokrasia na mafisadi kummaliza kabisa aliyekuwa Spika wa Bunge hilo, Samuel Sitta na kundi lake.
Habari za kuaminika kutoka vyanzo mbalimbali zimebainisha kuwa kile kilichotokea bungeni na kusimamiwa kikamilifu na Makinda ulikuwa ni utekelezaji wa matakwa ya wanasiasa na viongozi kadhaa wenye nguvu za fedha ambao waliumizwa vibaya na aina ya uongozi na maamuzi ya Sitta alipokuwa akikalia kiti hicho.
Inadaiwa kwamba mbali na kumkomoa, Makinda pia ameelekezwa kuhakikisha kuwa Sitta anamalizwa kisiasa, kwa kuwasulubu pia wabunge waliokuwa wakimuunga mkono, wakiwamo wale wa vyama vya upinzani hususan wa CHADEMA.
Moja ya chanzo chetu cha habari kimesema kuwa wanasiasa hao wakiwamo watendaji kadhaa wa serikali, walichukizwa na msimamo wa Sitta, hasa kusimamia ukweli na haki, na kuonekana kuwapendelea zaidi wabunge wa upinzani kuliko wale wa CCM.
Katika mkakati huo, iliamriwa kuwa nguvu zote alizotumia Sitta kuisulubu serikali na wanasiasa walioguswa masilahi yao, zivunjwe, likiwamo suala la kuunda na kuunganisha kamati ya hesabu za mashirika ya umma, na ya hesabu za serikali kuwa pamoja, kisha kuhakikisha inaongozwa na mbunge kutoka chama tawala.
Mbali na mipango hiyo, chanzo chetu kimesema kuwa mabadiliko hayo ya kamati yamefanywa kutokana na hofu ya kuumbuka kwa serikali kutokana na matumizi mabaya ya fedha, ikiwa kamati hizo zitaendelea kuwa chini ya wapinzani.
Katika mpango huo, Naibu Spika Ndugai, amejikuta akilazimika kukubaliana na maagizo ya mkuu wake wa kazi, licha ya ukweli kwamba ndiye alikuwa mwenyekiti wa kamati maalumu iliyoundwa katika Bunge la Tisa lililoongozwa na Sitta, ikiwa na lengo la kuleta mfumo mzuri wa utendaji wa Bunge, ikiwa ni pamoja na kurejesha hadhi yake ya kuiwajibisha serikali.
Ndugai katika kukamilisha azima ya Sitta, alilazimika na kamati yake iliyoundwa na wabunge wengine, Dk. Harrison Mwakyembe, Nimrod Mkono, Beatrice Shelukindo, Dk. Willibrod Slaa na Hamadi Rashid Mohamed, ilifanya ziara katika Bunge la Kenya, Uganda, India, Mauritius na Zimbabwe.
Kutokana na ziara hizo za mafunzo, Ndugai na kamati yake walipendekeza kutungwa kwa mambo yatakayolifanya Bunge lisimamie masilahi ya taifa badala ya vyama, vikao vyake kuoneshwa wazi kwa njia ya runinga ili wananchi waone na ripoti za mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali zijadiliwe na Bunge pamoja na kuondoa miswada yoyote iliyokuwa inaletwa kwa dharura bungeni.
Ni kamati ya Ndugai ndiyo ilipendekeza kuwa Kamati ya Mashirika ya Umma, (POAC), Kamati ya Serikali za Mitaa (LAAC) na Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) ziongozwe na upinzani ili kuongeza uwajibikaji wa serikali kwa Bunge.
Mbunge mmoja wa CCM ambaye amekuwa bungeni kwa muda mrefu (jina linahifadhiwa) alikiri kusikitishwa na uamuzi wa Spika Makinda, na kuonesha hofu ya kuvunjika kwa heshima na hadhi ya Bunge.
“Inasikitisha sana, maana sasa tunaelekea kuvunja hadhi ya Bunge na kulinda uozo wa serikali.
“Katika Bunge la Tisa, Sitta alijitahidi kuwa jasiri, kutopindisha ukweli ili kuilinda serikali, na alizielewa vizuri kanuni hasa ile ya 8 inayosema: “Hata kama Spika ametoka katika chama fulani anapaswa atende haki kwa pande zote,” alisema mbunge huyo.
Mbunge huyo alisema vurugu zilizotokea bungeni zilitokana na maamuzi mabaya ya kiti cha Spika, kinyume kabisa cha hotuba yake ya kwanza alipochaguliwa kushika wadhifa huo ya kuliunganisha Bunge kuwa moja.
Wakizungumza na Tanzania Daima Jumapili kwa njia ya simu, mmoja wa wajumbe wa iliyokuwa kamati ya Ndugai, Nimrodi Mkono, alisema hawezi kusema lolote kuhusiana na kuondolewa kwa kamati hizo, ingawa alikiri kuwa walichokishauri na kukubaliwa na Bunge kilikuwa cha maana na manufaa kwa taifa.
Kuhusiana na vurugu zilizotokea, Mkono alisema kelele za wapinzani zilikuwa sahihi hasa baada ya kuona kuwa wanaonewa, kutokana na uchache wao, hivyo kulazimika kupiga kelele ili hoja zao zisikiwe na Watanzania.
Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed, alishangaa kuunganishwa kwa Kamati ya Mashirika ya Umma pamoja na ile ya Hesabu za Serikali, huku akihoji kama Spika na wabunge wa CCM wapo tayari kuwa na mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti kutoka upinzani.
Akihojiwa kwa sharti la kutotajwa jina gazetini, kiongozi mmoja mashuhuri hapa nchini, amelaani aliouita uendeshaji mbovu wa shughuli za Bunge, na kuongeza kuwa kumetokana na udhaifu wa serikali yenye wabunge wasiojali masilahi ya taifa.
Alikwenda mbali zaidi na kudai kuwa kauli ya hivi karibuni ya Makinda wakati akitoa maoni mbele ya wajumbe wa kamati ya kukusanya maoni ya Katiba, ya kutaka Spika atoke nje ya chama, ilionesha kuwa huenda hata yeye analazimika kutekeleza maagizo na maelekezo ya chama na serikali yake hata kama hayataki.

[TD="bgcolor: #ffffff"]

na Josephat Isango

[/TD]
[TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF, align: center"]
amka2.gif
[/TD]

SITTA ALIKUWA SPIKA WA UKWELI!
 
  • Thanks
Reactions: MTK
Haya ni matokeo ya mtu mmoja kuwa na nguvu kubwa kisheria bila kuhojiwa ndio maana watu wanalalamikia sheria nyingi zilizopo zimekaa kama maandiko matakatifu kwamba hayahojiwi na hii ni hatari sana kwetu kama taifa.
Mnaweza mkakosana mnadani halafu mtu akakuletea matata kazini na asihojiwe na mamlaka yoyote. Inasikitisha!
 
Tuzidi kumuomba Mungu atujalie uzima, maana hadi 2015 tutaona mengi
 
Ukimfananisha na Makinda, kweli Sitta alikuwa Spika...
 
Ukilinganisha wakati wa Mhe Sita na sasa utaona mapungufu makubwa katika maamuzi ya waendeshaji na walindaji wa kanuni za bunge.

Mhe Makinda alichokosa katika utendaji wake ni hekima, busara na uadilifu katika kuliongoza Bunge. Mhe Ndugai anaweza kuwa miongoni mwa manaibu spika wabovu walioihujumu Bunge kwa sababu ya upendeleo, upofu na kutojali haki katika uendeshaji wa vikao. Historia itawahukumu hawa makada ambao hujinasibisha kama watetea haki lakini wakawa ndio wakuu wa upendeleo na mvurugo katika uendeshaji wa demokrasia ya nchi. Ipo haja tena ya dharura kwa uongozi wa Bunge kutopatikana kwa kupitia vyama ili heshima irejee na azma nzima ya transparency kupatikana.

On the other hand vyama vya upinzani vitaendelea kugeuzwa kama Omlet ikiwa havijaweka tafauti zao ili kupatikane nguvu za kweli, cuf, chadema, nccr, tlp etc vyote vinahitaji kuwaweka viongozi wao pamoja na kujadiliana area gani za kushirikiana na sio kila panapotokea tafauti kukimbilia vyombo vya habari kuhujumiana. Viongozi wa kweli wenye ari na hadhi ya kuitwa wanamageuzi huweka interest ya nchi kwanza kuhakikisha janga la sasa linatokomea. Naamini kwa dhati bila ya umoja wao hakutakuwa na mafanikio katika chaguzi zitazowaweka upinzani serikalini. Ondosheni tafauti zenu, kaeni wenyeviti muje na ari mpya na kasi ya juu ya kurejesha heshima ya nchi. Musikimbilie urais tu hebu jijengeni muweze kuwa na majority katika bunge kama kweli mumekusudia kuleta mabadiliko ya kweli, jengeni timu ya uhakika katika kila majimbo kuhakikisha upinzani unashika majority kubwqa katika bunge na hapo ndio utakuwa the begining of the end ya ubabe wa siasa za sasa, kung'ang'ania urais ni kuendeleza kugawiwa na kuhujumiana wenyewe kwa wenyewe..time to wake up and join the cause, together pamoja tutaweza.
 
Napenda kuamini kwamba CCM ni chama cha mapinduzi na sio CHAMA CHA MAZUZU!!

Kama hilo ni kweli basi wangekuwa wa kwanza kujifunza kutokana na historia kwamba wanamapinduzi wote maarufu duniani walionja shubiri ya mfumo tawala; jela kama kazi; baadhi walihasiwa na wengi waliuwawa lakini wengi wao waliibuka kidedea wakachukua hatamu za uongozi wa nchi zao na wengine wengi wanatambulika kama mashujaa wa kuigwa duniani kote.

Madiba, Jomo Kenyatta. Bob Mugabe bila kumsahau Baba yetu Mwalimu Nyerere na wengi wengineo walipitia barabara hiyo ya kadhia wakaibuka mashujaa.

Lakini ni kweli pia kwamba Haja ikiwa kubwa sana ya kufanya jambo; busara hudumaa ili mradi tu malengo yafikiwe; yawe mema au maovu kama haya uliyosimulia.

Juhudi zozote za kufifisha jina la Mzee wa kasi na viwango ni kumuongezea umaarufu; mfano mzuri ni jinsi Anna na Job wanavyopwaya kwenye kiti cha spika mpaka kuzomewa mbele ya kamera za runinga na kuwafanya watanzania wengi kumkubuka kwa upendo "nostalgia" Samwel Sitta alivyokimudu kiti kile kama alivyoahidi kwa "kasi na viwango"

Watanzania inatubidi tukubaliane na ukweli kwamba CCM na serikali yake watafanya kila wawezalo; jema au baya ili kulinda mfumo uliopo (Machiaveli na mabadiliko)

Changamoto tuliyonayo ni kukubali ukweli huo na kuongeza juhudi za kuuelimisha umma kuelekea ukombozi wa kweli na Tanzania tuipendayo kwa kutumia njia yoyote mbadala kulingana na matakwa ya wakati husika.

Siku zote haki haitolewi kwenye kisahani cha dhahabu bali hudaiwa na/au kupiganiwa If needs be! (Nelson Mandela; LONG WALK TO FREEDOM; The Rivonia Trial)

Walie wasage meno; waloge watambikie; CCM itan'goka tu; ni swala la lini sio kama!! kwa sababu huo ndio mkodo wa historia, They have outlived their useful life and now they must go; Hooks or Crooks.
 
Njia iliyobaki ni kuondoa udhibiti wa chama chochote katika bunge. Wingi wa wabunge wa CCM ndio unaotutesa.
 
Hivi hawa wanatumia mfumo gani,samweli sitta alikuwa na mfumo wa kasi na viwango.hakuwa kwa masilahi ya chama chochote anastaili hata kuwa raisi.
 
Tanzania daima na habari za masimulizi wapi na wapi???masimulizi haya hayakupashwa kuwa habari kuu ya gazeti chambuzi kama hili-mhariri-think twice.
 
Back
Top Bottom