Dotto C. Rangimoto
JF-Expert Member
- Nov 22, 2012
- 1,985
- 1,286
MAKENGEZA YA FIKRA
Unasema kwamba Lowassa anatuhumiwa tu kuhusu ufisadi hasa wa Richmond, na kwakuwa hajakutwa na hatia mahakamani hivyo anapaswa kuwa Raisi wa Tanzania, hapohapo unawalaumu wananchi wa Muleba kwa kumchagua Mama Anna Kajumulo Tibaijuka ambaye naye aliyetuhumiwa tu kuhusika na Sakata Escrow, tena yeye kwa kupokea fedha alizopewa, halafu tena wewe huyohuyo unawalalamikia wananchi waliowachagua watuhumiwa wengine kama Mtemi Chenge na wengineo, ambao nao kama ilivyo kwa mgombea wako wa Uraisi, hawajathibitika mahakamani kuhusika na ufisadi huo ? ?Makengeza ya Fikra?
Unawalalamikia na na hata kuwatusi wanaotumia haki yao ya msingi ya kufurahia kuangushwa kwa wagombea waliowadhihaki kama KAFULILA ati kisa kafulila alikuwa ana msimamo wa kutetea wananchi (hasa kwenye Escrow), wakati huohuo ulikuwa unasali usiku na mchana ukiomba Mungu Dr Mwakyembe aliyeisimamia vilivyo hoja ya RICHMOND ambayo iliwawajibisha wanaCCM wenzake akiwemo mgombea wako wa Uraisi, wewe huyohuyo unakesha usiku kucha ukiwa ?mtupu? ukitambika ili tu ZITTO KABWE aangushwe jimboni kwake huku ukifahamu fika kuwa kwa Kusimamia hoja zenye maslahi kwa umma ambazo zimeshaiwajibisha serikali mara kadhaa, Kafulila hafikii hata robo ya aliyoyafanya Zitto (ikiwemo na hiyohiyo Escrow).
Unawaambia wananchi wasifanye maamuzi kwa kuangalia mgogoro wa Zitto na Kafulila wakati wewe ulifanya maamuzi kwa Kuangalia mgogoro wa Zitto na ?akina Mbowe? ? ?Makengeza ya Fikra?
Uliziamini tuhuma kwamba Zitto aliisaidia NCCR dhidi ya chama chake cha zamani(CHADEMA) ili kumsaidia Kafulila aliyefukuzwa na Chadema, LEO unaziamini tena tuhuma kwamba Zitto ameisaidia CCM dhidi ya NCCR kwa ajili ya kumng?oa Kafulila wakati na yeye Zitto ana mgombea wa chama chake cha ACT hapo jimboni kwa Kafulia, wakati huohuo hautaki kuziamini tuhuma kwamba Kafulila ni miongoni mwa waliochangia mawazo na fedha juu ya kuanzishwa kwa ACT anayosema imeanzishwa na CCM ? ?Makengeza ya Fikra?
Unawatuhumu wapinzani wanaofurahia kuangushwa kwa WENJE wa CHADEMA na mgombea wa CCM, kuwa nao kwa ajili hiyo ni CCM pia, wakati huohuo nawe unafurahia kuangushwa kwa MACHALI wa ACT na mgombea wa CCM lakini wewe haujiiti CCM pia ? Hayo nayo ni Makengeza yaaa??? Eeeh ya Fikra.
Kufuatia kufutwa kwa matokeo ya Uchaguzi Zanzibar: WanaCCM wanafurahia maamuzi ya NEC kuendelea kutangaza matokeo ya Jamhuri ya Muungano kwakuwa wana dalili za kushinda, wanaUKAWA wa Zanzibar nao wanalilia matokeo yale ya awali yasifutwe kwakuwa wanaamini wameshinda, na wako radhi matokeo ya Jamhuri yaendelee kutangazwa hata kama yatamuangusha mwanaUKAWA mwenzao ilimradi wao wapate uRaisi kule visiwani ? Makengeza ya?.
Ubongo ukashakuwa na Makengeza, unaweza kuwa mara uone mbilimbili, mara ya kulia ije kushoto na kadhaaalika?!
Maundu Mwingizi
Mboka Manyemna