Make it Count,Make it Worth IT

tzhosts

JF-Expert Member
Nov 5, 2016
380
468
Habari za wakati huu,
Nimetumaini yangu kwamba mnaendelea vyema na majukumu ya ujenzi wa taifa.Leo ni tarehe 31 Ya mwisho wa mwaka.Leo nimeona nilete mjadala mdogo hasa kwetu sisi wajasiriamali na wafanya biashara.Natambua kwamba kuna ambao biashara zimewaendea vizuri kwa mwaka huu na kuna ambao zimeenda ndivyo sivyo.Kuna ambao mnataraji mwaka huu uwe bora na tofauti na kuna ambao mmekata tamaa.

Iko hivi.Unapoamua kuwa mjasiriamali au mfanya biashara umechangua fungu lililojema.Haijalishi biashara yako ni kubwa kiasi gani au ni ndogo kiasi gani ila umechagu kuwa chachu ya mabadiliko.Unapokuwa mjasiriamali unakuwa na uwezo wa kufanya jambo lolote kwa wakati wowote.

Najua kuna ambao hawataelewa ninachotaka kusema.Jeff Bezos,Elon Musk,Bill Gates,Zuckerberg,Altman,na Matajiri wengine wengi ambao wantishia Duniani kuna kipindi katika maisha yao walikuwa kama wewe au kama mimi.Walikuwa hawajui wafanye nini na walikuwa na hisia za kupoteza uelekeo au hata kuanguka na huo ndio wakati ambao iliwabidi au walilazimika kufanya maamuzi magumu.Iwapo upo katika nafasi ya chini katika maisha yako(LOWEST POINT) basi fahamu kwamba huo ndio muda wako muafaka wa kufanya maamuzi ambayo yatabadilisha kabisa maisha yako.

Fukara hapaswi kuwa na hofu ya kufilisika.Kuna hatua katika maisha hupaswi kuwa na hofu wala mashaka juu ya uelekeo wa maisha yako kwani na unachohitaji na kutambua kwamba hakuna cha kuogopa isipokuwa UOGA wako TU.

Mwaka Ujao unaweza kuwa mwaka wako wa mabadiliko na kuinuka.Kama ulikuwa unafanya biashara na ikawa haielekei kukulipa usiogope kubadili eneo la biashara,aina ya biashara au hata mfumo wa biashara.Kama ulikuwa umeajiriwa usiogope kutafuta kazi kampuni nyingine au hata kujiajri au kuanzisha kabiashara yako.Kama ulikuwa na Kipato cha ziada ambacho ulikitumia kwa anasa na matumizi yasiyo na TIJA usiogope sasa kuanza kuwekeza ama kwenye HIGH RISK venture au LOW RISK ventures.

Jambo la kuzingatia ni kuhakikisha kwamba mwaka 2023 unakuwa ulikufunza kitu ambacho 2024 itakuwa ni fursa yako ya kurekebisha.MAKE 2024 COUNT

Karibuni tujadili namna bora ya kufanya 2024 uwe mwaka SAHIHI KWETU Wapambanaji wadogo wadogo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom