Makazini Chunga kinywa si kila mtu rafiki yako

Pearce

JF-Expert Member
Dec 15, 2018
577
1,381
Kuna mshikaji mmoja ana cheo kunishinda kazini tuliwahi pishana pale kazini baada kumgundua alikuwa ananichafua kwa mameneja (ilitokea mazingira ya kupandishwa cheo kazini) ofisi ilinipendekeza. Kwahiyo akawa anawatumia watu tofauti nionekane sifai nina kiburi (ukweli mimi ni mtu mkimya)

Sasa bahati mbaya akiwa ananifanyia mikakati hiyo nilikuja fahamu kila kitu na bahati mbaya yeye akawa hajafahamu nimemtambua. Sema nikamkaushia nikawa naendelea na mambo yangu lakini naishi nae kwa akili sana.

Sasa majuzi tena akaenda nipaka uchafu mwingi kwa mameneja lakini nikapata nafasi ya kusikilizwa akagundulika yeye ana matatizo hayo hivyo lengo lake halikutimia nikabakizwa katika tasisi na yeye akawa kama kasusa. Akawapanga washkaji zake

Ambao ni kero anaweza kuja ofisini kwangu tukawa tunapiga story tu za maisha, lakini ajabu ataanza mtaja huyo mshikaji wake mbele zangu sasa mimi huwa na kwepa zungumzia chochote. Kikubwa huyu jamaa anaekuja ofisini kwangu ni moja ya watu ambao wanaopeleka sana maneno juu na nimemfahamu tayari.
 
Uzi tayari?

What if kweli wewe jeuri?umewahi waza Hilo since hakuna mtu jeuri anaekubali kuwa ni jeuri?.. hiko cheo ulipata?au ofisi imemkubali alichosema?
Sasa huyo anaekupa hizo Kazi na unamfanyia kazi zake vizuri mpaka unapata recommendation. Siamini mtu jeuri anaweza kuwa Subordinate kwenye tasisi yoyote
 
Uzi tayari?

What if kweli wewe jeuri?umewahi waza Hilo since hakuna mtu jeuri anaekubali kuwa ni jeuri?.. hiko cheo ulipata?au ofisi imemkubali alichosema?
Kifupi haikumkubalia sababu at the end Alishawahi misbehave pia kwa wakuu kazini na kuwafanyia wengine walio chini yake akafanikiwa. Akarudi attempt kwangu sababu nilikuwq namkwepa.

Bahati mbaya hao jamaa waliondolewa
 
Kuna mshikaji mmoja ana cheo kunishinda kazini tuliwahi pishana pale kazini baada kumgundua alikuwa ananichafua kwa mameneja (ilitokea mazingira ya kupandishwa cheo kazini) ofisi ilinipendekeza. Kwahiyo akawa anawatumia watu tofauti
Daah kwa hio ikawaje mkuu story haijaisha au tusubiri next episode nahofia usije ukapigwa pin huku episode haijaishi watu wataanza kusumbua,

Ndio imeishia hapo kweli mkuu?
 
Kenge anaishi vipi
Kivyake vyake ni ngumu kuona wakiishi kwenye jumuiya isipokuwa muda wa kupandana.

Hujiepusha na shida nyingi na hapendi tabu yaani hadi matone ya mvua yeye hukimbilia mtoni.

Kifupi kwenye maofisi ukiwa threat kwa superior wako.
Kwa ufanisi, vigezo vya elimu, experience basi jiandae kuingia kwenye shida na yeye kutokukusema vizuri kule juu.

Ishi kikenge na kumbuka kanuni kumi(10) za subordinate kwa superior wake.

La mwisho jifunze udhaifu wake na kumbuka hakuna binadamu asiye na udhaifu, kumbuka Dunia ni unafiki tu.
 
Ukiona mtu anakuspoil kwa mkuu wako ujue anaudhaifu flan kweny weledi wake wa kazi kwa hyo anajarbu kujifichia hapo kwa kupeleka taarifa mbaya kwa mabosi ili wasifocus kwake zaid ila waje kwako ambaye unafanya kazi nzur..
Tatizo Kuna kitu kinaitwa character Assassination yaani wanaharibu sifa na wajihi wako.

Watu watakuogopa bila kujua tabia zako, na ukifanya masikhara utahamishwa mbali , au hata mizengwe ya kufukuzwa kazi
 
Kivyake vyake ni ngumu kuona wakiishi kwenye jumuiya isipokuwa muda wa kupandana.

Hujiepusha na shida nyingi na hapendi tabu yaani hadi matone ya mvua yeye hukimbilia mtoni.

Kifupi kwenye maofisi ukiwa threat kwa superior wako.
Kwa ufanisi, vigezo vya elimu, experience basi jiandae kuingia kwenye shida na yeye kutokukusema vizuri kule juu.

Ishi kikenge na kumbuka kanuni kumi(10) za subordinate kwa superior wake.

La mwisho jifunze udhaifu wake na kumbuka hakuna binadamu asiye na udhaifu, kumbuka Dunia ni unafiki tu.
Mkuu naomba haya maneno niyaprint niweke ukutani
 
Tatizo Kuna kitu kinaitwa character Assassination yaani wanaharibu sifa na wajihi wako.

Watu watakuogopa bila kujua tabia zako, na ukifanya masikhara utahamishwa mbali , au hata mizengwe ya kufukuzwa kazi
Mkuu ameshafanya sana hicho na kuna jamaa alisababisha wakapigwa chini, Mimi niseme tu Mungu ananisaidiaga anapotumia nguvu hiyo lakini wakubwa wanaponikaribia na kuona utendaji wangu wa kazi wananiacha sababu hawaoni kosa lolote.

Kingine nimempita Kielimu, Na pale kazini kutokana na muonekano wangu hutokea Staff wakike kunipenda na so often namuona anaumia na icho

Kifupi kanitengenezea maadui wengi sana ingawa naamini katika kukaa kimya na kutojali sana zaidi ya kutimiza majukumu yangu na ubunifu wa kutatua changamoto au maboresho kikazi kitu kinachonifanya mabosi wanipende.
 
Kuna mshikaji mmoja ana cheo kunishinda kazini tuliwahi pishana pale kazini baada kumgundua alikuwa ananichafua kwa mameneja (ilitokea mazingira ya kupandishwa cheo kazini) ofisi ilinipendekeza. Kwahiyo akawa anawatumia watu tofauti nionekane sifai nina kiburi (ukweli mimi ni mtu mkimya)

Sasa bahati mbaya akiwa ananifanyia mikakati hiyo nilikuja fahamu kila kitu na bahati mbaya yeye akawa hajafahamu nimemtambua. Sema nikamkaushia nikawa naendelea na mambo yangu lakini naishi nae kwa akili sana.

Sasa majuzi tena akaenda nipaka uchafu mwingi kwa mameneja lakini nikapata nafasi ya kusikilizwa akagundulika yeye ana matatizo hayo hivyo lengo lake halikutimia nikabakizwa katika tasisi na yeye akawa kama kasusa. Akawapanga washkaji zake

Ambao ni kero anaweza kuja ofisini kwangu tukawa tunapiga story tu za maisha, lakini ajabu ataanza mtaja huyo mshikaji wake mbele zangu sasa mimi huwa na kwepa zungumzia chochote. Kikubwa huyu jamaa anaekuja ofisini kwangu ni moja ya watu ambao wanaopeleka sana maneno juu na nimemfahamu tayari.
Kaka inawezekana kabisa wewe unaonewa, ila ni vizuri pia kujitafakari. Unaweza ukawa na vitu vinavyokufanya victim, mfano arrogance. Hayo mambo ni kawaida maofisini, ila kuna wakati unapaswa kuchukulia positive na kujitafakari kama uko sawa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom