Makazi Ya Viongozi Uswahilini vs Usalama,Ulinzi

mwanamichakato

JF-Expert Member
Mar 20, 2015
1,169
1,073
Kuuzwa kwa nyumba za serikali na hasa za viongozi kunasababisha usumbufu mkubwa sana kwa viongozi waandamizi walioendelea kuteuliwa na kuchaguliwa kwa miongo kadhaa katika hatamu mbalimbali za kiuongozi mara baada ya awamu ya tatu..

Imefika wakati viongozi nyeti na waandamizi kuwa wanaishi katika makazi yao binafsi yalio katika maeneo dhaifu na yasio bora kiusalama na vinginevyo.Misafara ya ving'ora vyenye kustua mioyo kila siku kuingia na kutoka makazi yao huku uswahilini ni mojawapo ya mfumo mpya wa kwenda na kurudi kwa hawa waandamizi..Mfano mzuri ni Mh Spika,Naibu Spika,CDF,etc

Ipo haja ya Serikali kuangalia uwezekano wa hata ikibidi kuzinunua upya nyumba iliowauzia waliokuwa watumishi wa serikali katika maeneo yenye miundombinu ya kiulinzi na kiusalama lakini ilio karibu na maeneo ya utekelezaji wa majukumu ya viongozi husika.

Mchakato wa kuhamia dodoma pia uzingatie kwa kiwango kikubwa ujenzi wa makazi maalumu ya viongozi wa juu,kati na chini na pia zuio la kuuza mali za taifa {makazi} liwekwe katika katiba ili kuepusha miemuko ya kimaamuzi ya viongozi wa kisiasa sasa na tuendako...
 
Back
Top Bottom